Uingereza: Hatutaingia katika vita dhidi ya Iran/ Ireland yalaani uvamizi wa Marekani na Wazayuni dhidi ya Iran
-
Yvette Cooper
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza amesema kuwa London haitajiunga katika vita vya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Iran.
Yvette Cooper amesisitiza kwamba London inajiepusha kuingia katika mzozo wa Magharibi mwa Asia. Cooper amesema: “Tumepata funzo kutokana na vita vya Iraq na tutatumia uzoefu huo katika vita vya sasa.”
Wakati huo huo Sadiq Khan, Meya wa jiji la London amesema vita dhidi ya Iran bila ya mwafaka wa kimataifa haina idhini ya Umoja wa Mataifa; na Uingereza haipasi kuingia katika vita hivyo. Amesema, vita dhidi ya Iran huwenda vikatikisa pakubwa uchumi wa Uingereza.
Katika upande mwingine na katika kuendeleaa wimbi la upinzani wa kulaani vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran, Rais wa Jamhuri ya Ireland, Catherine Connolly amevitaja vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran kuwa ni jinai na kusisitiza kuwa, matukio ya hivi karibuni katika eneo la Magharibi mwa Asia ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa na hati ya Umoja wa Mataifa.
Naye Mary Robinson rais wa zamani wa Ireland ameituhumu serikali ya Donald Trump nchini Marekani kuwa inaeneza uongo.
Amesema: hivi sasa tunashuhudia vita vilivyoanzishwa na Israel na Marekani dhidi ya Iran na vita hivi vimesababisha uharibifu mkubwa katika eneo la Asia Magharibi.