Uhispania: Kamisheni ya Ulaya itetee sheria za kimataifa/ Wallace: Muungano wa Epstein unalenga raia nchini Iran
https://parstoday.ir/sw/news/world-i137266-uhispania_kamisheni_ya_ulaya_itetee_sheria_za_kimataifa_wallace_muungano_wa_epstein_unalenga_raia_nchini_iran
Naibu Waziri Mkuu wa Uhispania amekosoa vikali matamshi ya Mkuu wa Kamisheni ya Ulaya, Ursula von der Leyen, kuhusu utaratibu wa kimataifa na kuunga mkono vita vya uvamizi dhidi ya Iran.
(last modified 2026-03-10T10:24:40+00:00 )
Mar 10, 2026 10:24 UTC
  • Yolanda Díaz
    Yolanda Díaz

Naibu Waziri Mkuu wa Uhispania amekosoa vikali matamshi ya Mkuu wa Kamisheni ya Ulaya, Ursula von der Leyen, kuhusu utaratibu wa kimataifa na kuunga mkono vita vya uvamizi dhidi ya Iran.

Ursula von der Leyen Mkuu wa Kamisheni ya Ulaya Jumatatu wiki hii alisema kuwa anaunga mkono mtazamo kwamba Ulaya inahitaji "sera ya kigeni ya uhakika zaidi na inayozingatia maslahi" iliyo juu zaidi ya "utaratibu wa zamani wa dunia" unaotegemea sheria na nidhamu ya kimataifa. Ameongeza kuwa: “Tunasikia maoni tofauti juu ya iwapo vita dhidi ya Iran ni vita ya kujitakia au vita vya udharura. Ninaamini mijadala hii inapuuza nukta kwamba Ulaya inapasa kuzingatia uhakika wa hali halisi ya sasa na tunapaswa kuiona dunia kama ilivyo hii leo.”

Naibu Waziri Mkuu wa Uhispania, Yolanda Díaz, amekosoa vikali matamshi haya ya Mkuu wa Kamisheni ya Ulaya, Ursula von der Leyen kuhusu nidhamu ya kimataifa na kuunga mkono wa vita vya kichokozi dhidi ya Iran.

Díaz, ambaye ni mkuu wa chama cha mrengo wa kushoto cha Somar katika serikali ya muungano ya Uhispania, amesisitiza: "Vita hivi ni kinyume cha sheria na vinakiuka Mkataba wa Umoja wa Mataifa." Ameongeza kuwa: Kwa hiyo, ninamtaka Mkuu wa Kamisheni ya Ulaya kutetea sheria za kimataifa.

Katika upande mwingine, Mick Wallace mwakilishi wa zamani katika Bunge la Ulaya amesema Ulaya inafumbia macho jinai za kivita zinazofanywa Marekani na Israel nchini Iran. Wallache jana Jumatatu aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii X kwamba: "Muungano wa Epstein-Marekani na Israel unawalenga raia nchini Iran, na Umoja wa Ulaya haujali suala hilo.”

Wallace ameongeza: "Mataifa ya Magharibi yameweka kando sheria za kimataifa, ni aibu iliyoje kwa mataifa haya."