Wall Street Journal: Kambi ya Diego Garcia imeshambuliwa kwa makombora ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/world-i137496-wall_street_journal_kambi_ya_diego_garcia_imeshambuliwa_kwa_makombora_ya_iran
Gazeti la Kimarekani la Wall Street Journal limeripoti kwamba, Iran imeshambulia kwa makombora mojawapo ya kambi za mbali zaidi za kistratijia za jeshi la Marekani nje ya nchi hiyo.
(last modified 2026-05-10T14:24:40+00:00 )
Mar 21, 2026 06:36 UTC
  • Kambi ya kijeshi ya Diego Garcia iliyoko Bahari ya Hindi
    Kambi ya kijeshi ya Diego Garcia iliyoko Bahari ya Hindi

Gazeti la Kimarekani la Wall Street Journal limeripoti kwamba, Iran imeshambulia kwa makombora mojawapo ya kambi za mbali zaidi za kistratijia za jeshi la Marekani nje ya nchi hiyo.

Televisheni ya al Jazeera ya Qatar imelinukuu gazeti la Wall Street Journal kwamba Jamhuri ya Kiislamu imepiga kambi ya kijeshi ya Diego Garcia iliyoko Bahari ya Hindi kwa kutumia makombora mawili ya balestiki.

Baada ya Wall Street Journal kufichua habari hiyo, maafisa wa Marekani wamedai kuwa mashambulizi hayo ya makombora hayakusababisha hasara za roho.

Ripoti ya Wall Street Journal imesema, kambi ya kijeshi ya Diego Garcia ya majeshi ya Marekani na Uingereza iliyolengwa kwa makombora ya Iran iko umbali wa karibu kilomita elfu nne kutoka kwenye ardhi ya Iran.

Ripoti zinasema tukio hilo linadhihirisha uwezo wa makombora ya Iran wa kuweza kulenga shabaha maeneo ya mbali ya adui.   

Awali, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran alitetea hatua za kujitetea za Iran mkabala wa mashambulizi ya Marekani na Israel katika mazungumzo yake ya simu na mwenzake wa Uingereza, Yvette Cooper, na kukosoa msimamo hasi na wa upendeleo wa London na baadhi ya nchi za Ulaya kuhusu mashambulizi hayo ambayo yamekiuka sheria za kimataifa.

Sayyid Abbas Araqchi amekosoa vikali hatua ya Uingereza ya kuipatia Marekani kambi zake za kijeshi kwa ajili ya kuendeleza mashambulizi dhidi ya Iran. Ameongeza kuwa bila shaka yoyote kitendo hicho ni kushiriki katika mashambulizi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu na kitasajiliwa katika historia ya uhusiano wa nchi mbili.