Waziri Mkuu wa Uhispania ataka kulindwa vyanzo vya nishati katika Mashariki ya Kati
-
Pedro Sanchez
Waziri Mkuu wa Uhispania ametahadharisha kuhusu mgogoro wa nishati wa muda mrefu kwa wanadamu wote kutokana na vita vya uchokozi vya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Iran na kutaka kulindwa vyanzo vyote vya nishati katika eneo la Mashariki ya Kati.
Pedro Sanchez ametuma ujumbe katika akaunti yake ya X akisisitiza kuwa: "Tumo katika kipindi nyeti na sana katika upeo wa kimataifa."
Amesisitiza kuwa kushtadi zaidi mapigano kunaweza kuibua mgogoro wa nishati wa muda mrefu kwa wanadamu wote. Waziri Mkuu wa Uhispania ametaka kufunguliwa Lang Bahari la Hormuz na kulindwa vyanzo vyote vya nishati katika Mashariki ya Kati na kuongeza kuwa: Ulimwengu haupasi kulipa gharama za vita hivi.
Sanchez ameyataja mashambulizi ya kijeshi ya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Iran kuwa kinyume cha sheria na kwamba yanayumbisha amani na kusisitiza kuwa: Kwa sababu hii tunapinga vita hivi.
Ameongeza kuwa: Tumeshuhudia jinsi vita hivi vilivyosababisha hasara kubwa.
Shirika la habari la IRNA limeripoti kuwa, baada ya Rais wa Marekani kutishia kushambulia miundo mbinu ya nishati ya Iran; Msemaji wa Makao Makuu ya Jeshi ya Khatamul Anibiyaa alimtahadharisha papo hapo adui Marekani na Mzayuni kwamba: Miundo mbinu yote ya Marekani na utawala wa Kizayuni katika eneo la Magharibi mwa Asia itashambuliwa iwapo pande hizo mbili zitashambulia miundo mbinu ya mafuta na nishati ya Iran.
Mashambulizi ya kijeshi ya pamoja ya Marekani na utawala wa Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yaliyomuuwa shahidi Ayatullah Ali Khamenei yalianza asubuhi ya tarehe 28 Februari mwaka huu. Marekani na Israelizimeanzisha mashambulizi hayo dhidi ya Iran wakati Iran na Marekani zikiwa katika mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kwa upatanishi wa baadhi ya nchi za kanda hii.
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa upande wake imetoa jibu kali kwa mashambulizi ya kijeshi ya Marekani na Israel.
Iran imeshambulia maeneo ya kijeshi na kiusalama ya utawala wa Kizayuni katika miji mbalimbali ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu na pia kambi za kijeshi na vituo vya wanajeshi wa Marekani katika eneo la Magharibi mwa Asia kwa kuvurumisha makombora, ndege zisizo na rubani na mashambulizi ya anga kwa kulenga kwa usahihi shabaha zilizokusudiwa katika fremu ya jibu halali la Iran mkabala wa uvamizi wa Marekani na Israel.