Kinara wa Liberal Democrats Uingereza asema Trump ni jambazi fisadi na hatari
https://parstoday.ir/sw/news/world-i137846-kinara_wa_liberal_democrats_uingereza_asema_trump_ni_jambazi_fisadi_na_hatari
Mwanasiasa wa Uingereza amemtaja Donald Trump, rais wa Marekani, kuwa jambazi fisadi na hatari, na kusisitiza kuwa kitendo chake cha kuzingira Mlango-Bahari wa Hormuz kinaweza kuhatarisha usitishaji mapigano dhaifu kati ya Tehran na Washington.
(last modified 2026-04-15T08:16:29+00:00 )
Apr 15, 2026 08:12 UTC
  • Donald Trump
    Donald Trump

Mwanasiasa wa Uingereza amemtaja Donald Trump, rais wa Marekani, kuwa jambazi fisadi na hatari, na kusisitiza kuwa kitendo chake cha kuzingira Mlango-Bahari wa Hormuz kinaweza kuhatarisha usitishaji mapigano dhaifu kati ya Tehran na Washington.

Edward Davey, kiongozi wa Chama cha Liberal Democrats nchini Uingereza, katika hotuba yake kwenye Bunge la Commons, amekosoa uchochezi wa vita wa Donald Trump dhidi ya Iran na kutaka kufutwa safari ya Mfalme wa Uingereza kwenda Marekani.

Katika sehemu ya hotuba yake Davey amesema: “Trump amesema kuwa ataharibu ustaarabu mzima wa Iran. Sikuwahi kufikiri nitasikia maneno kama haya kutoka kwa rais wa Marekani. Maneno haya yanakumbusha waziwazi jinsi rais huyu wa Marekani anavyotenda bila kijali lolote, bila maadili na nje kabisa ya mipaka ya sheria za kimataifa. Yeye si rafiki wa Uingereza, si kiongozi wa dunia huru; Trump ni ‘jambazi hatari na fisadi.’”

Mbunge huyo pia ameongeza kuwa kwa hali hiyo, uamuzi wa Uingereza kutoshirikiana na Trump katika vita dhidi ya Iran ulikuwa sahihi.Wakati huohuo, Giorgia Meloni, Waziri Mkuu wa Italia, katika hatua isiyo ya kawaida, amemkosoa Donald Trump kwa kumvunjia heshima kiongozi wa Wakatoliki duniani, akisema: “Haikubaliki kutoa maneno kama hayo kuhusu kiongozi mtakatifu. Papa ni kiongozi wa Kanisa Katoliki, na ni jambo la kawaida kwake kutaka amani na kulaani vita vyovyote.”

Naye Bernie Sanders, seneta wa kujitegemea wa Marekani, pia ameandika kwenye mitandao ya kijamii akisema: “Trump sasa anamvamia Papa, ambaye amepinga vita waziwazi, na wakati huohuo anachapisha picha yake kama Yesu Mwokozi. Hili sio tu tusi, bali ni ishara ya kujiona kupita kiasi na matatizo ya kisaikolojia. Warepublican wataendelea kumfuata mtu huyu mwendawazimu na hatari mpaka lini?”

Papa Leo wa XIV hivi karibuni alikosoa vitisho vya Donald Trump, rais wa serikali ya Marekani ambayo inatuhumiwa kwa ugaidi wa kiserikali, kuhusu kuangamiza ustaarabu wa Iran na uvamizi wa kijeshi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu. Akijibu matusi ya Trump wakati alipoulizwa kuhusu ukosoaji wake dhidi ya uvamizi unaofanywa na Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran, Papa alisisitiza: “Sitishwi na serikali ya Trump.”