Makundi ya Kiislamu ya Marekani yatoa wito wa kuwachiwa huru kiongozi wa jumuiya ya Wapalestina
https://parstoday.ir/sw/news/world-i137876-makundi_ya_kiislamu_ya_marekani_yatoa_wito_wa_kuwachiwa_huru_kiongozi_wa_jumuiya_ya_wapalestina
Muungano wa mashirika ya kutetea haki za kiraia ya Kiislamu Jumatatu wiki hii ulikusanyika nje ya Mahakama ya Juu ya Marekani ukitaka kuachiwa huru haraka iwezekanavyo Salah Sarsour, kiongozi wa Jumuiya ya Wapalestina huko Milwaukee ambaye anaishi Marekani kwa zaidi ya miaka 30.
(last modified 2026-04-21T09:15:40+00:00 )
Apr 21, 2026 09:05 UTC
  • Makundi ya Kiislamu ya Marekani yatoa wito wa kuwachiwa huru kiongozi wa jumuiya ya Wapalestina

Muungano wa mashirika ya kutetea haki za kiraia ya Kiislamu Jumatatu wiki hii ulikusanyika nje ya Mahakama ya Juu ya Marekani ukitaka kuachiwa huru haraka iwezekanavyo Salah Sarsour, kiongozi wa Jumuiya ya Wapalestina huko Milwaukee ambaye anaishi Marekani kwa zaidi ya miaka 30.

Sarsour anashikiliwa na Idara ya Uhamiaji na Forodha ya Marekani (ICE) tangu Machi 30 mwaka huu.

Salah Sarsour, ambaye ni mkuu wa Jumuiya ya Kiislamu ya Milwaukee na mjumbe wa bodi ya Waislamu wa Marekani kwa ajili ya Palestina, tarehe 30 mwezi Machi mwaka huu aliburutwa na zaidi ya mawakala 10 wa polisi wa Idara ya Uhamiaji na Forodha ya Marekani (ICE) alipokuwa akiendesha gari karibu na nyumba yake.

Awali Salah Sarsour alipelekwa katika korokoro ya idara ya ICE huko Chicago kabla ya kuhamishwa katika korokoro nyingine huko Indiana. 

Bodi ya Waislamu wa Marekani kwa Ajili ya Palestina imesema kuwa Salsour ni mkazi halali wa kudumu nchini Marekani kwa zaidi ya miaka 32.

Mashirika mbalimbali yakiwemo CAIR, Baraza la Mashirika ya Kiislamu ya Marekani na mashirika mengine pia jana yaliitisha mkutano na waandishi wa habari yakitaka kuachiwa huru Salah Sarsour. Mashirika hayo yamesema kuwa Salsour amelengwa kwa sababu ya kutetea Palestina.