Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani wa Austria: Iran sasa ni dola kubwa lenye ushawishi
https://parstoday.ir/sw/news/world-i139692-waziri_wa_mambo_ya_nje_wa_zamani_wa_austria_iran_sasa_ni_dola_kubwa_lenye_ushawishi
Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Austria amesema, akiashiria nafasi ya ustaarabu wa maelfu ya miaka wa Iran katika historia ya dunia, kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa sasa imegeuka kuwa moja ya mataifa makubwa yenye ushawishi katika ngazi ya kimataifa.
(last modified 2026-07-11T07:59:36+00:00 )
Jul 07, 2026 03:25 UTC
  • Karin Kneissl
    Karin Kneissl

Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Austria amesema, akiashiria nafasi ya ustaarabu wa maelfu ya miaka wa Iran katika historia ya dunia, kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa sasa imegeuka kuwa moja ya mataifa makubwa yenye ushawishi katika ngazi ya kimataifa.

Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Austria amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sasa inatambuliwa kama moja ya vituo vikuu vya nguvu katika mfumo wa dunia wa pande nyingi, akisisitiza kuwa nchi hiyo imeonyesha ustahimilivu wa hali ya juu mbele ya mashambulizi ya Marekani.

Kwa mujibu wa Pars Today ikinukuu IRNA, Karin Kneissl, Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Austria, amesema katika mahojiano kuwa, Iran kwa sasa imejidhihirisha kama nguvu muhimu katika dunia yenye mfumo wa pande nyingi, baada ya kuonyesha uwezo mkubwa wa kustahimili uchokozi wa Marekani.

Kneissl ameongeza kuwa nafasi mpya ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mlingano wa kisiasa wa kimataifa imezua wasiwasi mkubwa mjini Washington.

Katika kauli nyingine alizowahi kuzitoa, Kneissl alisisitiza kuwa Marekani haiwezi kudai kuwa ilipata ushindi katika vita dhidi ya Iran, akieleza kuwa, hadhi na uaminifu wa jeshi la Marekani umewekwa katika mtihani mkubwa.

Aidha, amesema kuwa juhudi za Marekani na utawala wa Kizayuni za kuishinda Iran hazikufanikiwa, akibainisha kuwa licha ya mashambulizi ya Marekani na Israel, muundo wa dola na taasisi kuu za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zimeendelea kubaki imara.