Trump anazidi kuchanganyikiwa kuhusu ulipizaji kisasi wa Iran, amkabili Hegseth kuhusu uhaba wa silaha
-
Trump na Hegseth
Rais wa Marekani, Donald Trump, amezidi kukatishwa tamaa na kushindwa mara kwa mara kwa mashine ya kivita ya nchi hiyo kutokana na ulipizaji kisasi wa Iran na amemkabili Waziri wa Vita, Pete Hegseth, kuhusu uhaba wa silaha muhimu za Marekani.
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na The Washington Post jana Jumatano, mzozo baina ya Trump na Hegseth uliibuka huko Camp David Ijumaa iliyopita, ambapo Trump alitaka kupata majibu kutoka kwa waziri wake wa vita, Pete Hegseth kuhusu ni kwa nini inaonekana amepewa "picha isiyo sahihi" ya uwezo wa kijeshi wa Marekani, huku Washington ikikabiliwa na uhaba wa makombora ya masafa marefu na mitambo ya ulinzi wa anga.
Uhaba huo umekuwa kikwazo kwa machaguo ya kijeshi ya Marekani, huku nchi hiyo ikiwa na upungufu wa zana za ulinzi ikiwa ni pamoja na upungufu wa mfumo wa ulinzi wa anga wa THAAD, ili kulinda wanajeshi wa Marekani walioko kwenye vituo na kambi ambazo zimeathiriwa kwa mashambulizi makali ya Iran.
Kwa mujibu wa watu wawili wanaojua vyema hali hiyo ambao wamenukuliwa na The Post, kuchanganyikiwa kwa Trump kuhusu hali hiyo kuliongezeka wakati wa mkutano wa Baraza la Mawaziri.
Mzozo huo ulifikia kilele baada ya kuibuka swali kwamba "kwa nini Hegseht amepotoshwa kuhusu uhaba mkubwa wa silaha ambazo sasa zinatishia kupunguza machaguo ya kijeshi kuhusiana na Iran," vyanzo hivyo vimeliambia gazeti hilo.
Inaripotiwa kwamba Hegseth alimtupia lawama za uhaba huo na kushindwa kuwasilisha zana za kutosha Naibu Waziri wa Vita, Stephen Feinberg.
Kupungua kwa mifumo wa ulinzi wa anga ya THAAD kunapewa mazingatio makubwa sana na vikosi vya jeshi la Marekani, ikizingatiwa kwamba mashambulizi ya Iran yamekuwa yakiwalenga maafisa na kambi za kijeshi za Marekani katika eneo lote la Magharibi mwa Asia na hadi sasa yameangamiza mamia ya wanajeshi kwa mujibu wa takwimu za Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (IRGC), ingawa vyombo vya habri vya Magharibi na washirika wao vinavicha takwimu hizo.