Telegraph: Vita dhidi ya Iran vinaweza vikawa moja ya makosa ya kihistoria
https://parstoday.ir/sw/news/world-i140496-telegraph_vita_dhidi_ya_iran_vinaweza_vikawa_moja_ya_makosa_ya_kihistoria
Gazeti la Telegraph linalochapishwa nchini Uingereza limekiri katika ripoti yake kwamba Marekani na Israel zimeshindwa katika vita, huku Iran ikiwa imeibuka mshindi, na kwamba vita hivi vinaweza kuwa tukio muhimu sana la kupelekea kupungua satua na ushawishi wa Marekani duniani.
(last modified 2026-08-08T03:24:16+00:00 )
Aug 08, 2026 03:22 UTC
  • Telegraph: Vita dhidi ya Iran vinaweza vikawa moja ya makosa ya kihistoria

Gazeti la Telegraph linalochapishwa nchini Uingereza limekiri katika ripoti yake kwamba Marekani na Israel zimeshindwa katika vita, huku Iran ikiwa imeibuka mshindi, na kwamba vita hivi vinaweza kuwa tukio muhimu sana la kupelekea kupungua satua na ushawishi wa Marekani duniani.

Telegraph limebainisha katika ripoti kwamba makubaliano ambayo yanaweza kufikiwa kati ya Iran na Oman kuhusiana na Mlango-Bahari wa Hormuz yanaonyesha kuwa Tehran imeibuka kutoka kwenye mzozo huu ikiwa na nguvu zaidi kuliko ilivyokuwa hapo awali.

Ripoti ya gazeti hilo la Uingereza imeendelea kueleza kwamba, vita ambavyo Trump na Netanyahu walivianzisha ili kuipindua au kuidhoofisha Jamhuri ya Kiislamu vimemalizika kwa kupanuka kwa uwazi kabisa ushawishi wa kikanda wa Iran. Marekani na Israel zimeshindwa katika vita hivi, huku Iran ikiibuka mshindi.

Telegraph limeongezea kwa kueleza: Mikataba ya suluhu huwa mwishowe ndiyo inayoakisi matokeo ya mapigano kwenye medani ya vita ambayo Washington ilijaribu na ikashindwa kuyabadilisha.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, vita dhidi ya Iran vinaweza vikawa moja ya makosa ya kihistoria.

Gazeti la Telegraph limesisitiza kwamba kuna uwezekano wa mgogoro wa sasa na Iran ukawa tukio muhimu katika la kupelekea kupungua ushawishi wa Marekani duniani…/