Russia yashambulia eneo la kutengeneza makombora na ghala la mafuta la Ukraine huko Kyiv
https://parstoday.ir/sw/news/world-i140504-russia_yashambulia_eneo_la_kutengeneza_makombora_na_ghala_la_mafuta_la_ukraine_huko_kyiv
Wizara ya Ulinzi ya Russia imetangaza kuwa vikosi vya ulinzi ya nchi hiyo vimeshambulia kituo cha kijeshi na viwanda cha Ukraine kinachotengeneza makombora ya cruise pamoja na ghala la mafuta huko Kyiv.
(last modified 2026-09-03T12:21:49+00:00 )
Aug 08, 2026 12:46 UTC
  • Mashambulizi ya Russia dhidi ya Ukraine
    Mashambulizi ya Russia dhidi ya Ukraine

Wizara ya Ulinzi ya Russia imetangaza kuwa vikosi vya ulinzi ya nchi hiyo vimeshambulia kituo cha kijeshi na viwanda cha Ukraine kinachotengeneza makombora ya cruise pamoja na ghala la mafuta huko Kyiv.

Katika taarifa yake ya mapema leo Jumamosi, wizara hiyo imetangaza kuwa mashambulizi hayo yaliyohusisha silaha za nchi kavu zinazolenga kwa usahihi yamelenga kiwanda nambari 111 katika mji mkuu wa Ukraine, Kyiv ambacho huzalisha vipuri na vichwa vya makombora yanayorushwa kutoka katika meli aina ya "FP-5 Flamingo".

Wizara ya Ulinzi ya Russia imeeleza kuwa kiwanda hicho kilikuwa kikiendeshwa na Kampuni ya Fire Point, iliyopigiwa debe kimataifa na Vladimir Zelensky wa Ukraine na kinachohusishwa na mfanyabiashara mwenzake wa zamani, Timur Mindich, ambaye ni mtu muhimu katika kashfa kubwa ya ufisadi.

Jeshi la Russia pia limeripoti kuwa limeshambulia ghala la mafuta la Kiev-3 linalomilikiwa na kampuni ya Grand-terminal, ambalo linasambaza bidhaa za petroli kwa jeshi la Ukraine.

Inaripotiwa kuwa malori ya mafuta yalitumwa kutoka kituo hicho ili kupeleka mafuta kwa wanajeshi wa Ukraine mashariki mwa nchi hiyo.

Kwingineko, Wizara ya Ulinzi ya Russia imetangaza kuwa droni za nchi hiyo zimezishambulia meli mbili za mizigo baharini kusini na mashariki mwa Odessa.

Meli hizo zilikuwa zikisafirisha zana na vifaa vingine vya kijeshi hadi katika bandari za Ukraine.

Katika wiki za hivi karibuni, jeshi la Russia limezidisha mashambulizi ya masafa marefu dhidi ya viwanda vya Ukraine vinavyozalisha vifaa vinavyotumika jeshini na katika miundombinu muhimu kwa ajili ya matumizi ya kiraia na ulinzi.