Jenerali wa Trump anatafuta njia ya kujiondoa vitani na Iran huku machaguo ya kijeshi ya Marekani yakipungua
https://parstoday.ir/sw/news/world-i140516-jenerali_wa_trump_anatafuta_njia_ya_kujiondoa_vitani_na_iran_huku_machaguo_ya_kijeshi_ya_marekani_yakipungua
Mkuu wa Majeshi ya Marekani, Jenerali Daniel Caine, amewasihi maafisa wakuu wa utawala wa Trump kutafuta njia ya kupunguza vita na Iran, akionya kwamba ongezeko zaidi la mapigano ya kijeshi haliwezi kupata mafanikio makubwa na kwamba linawaweka wanajeshi wa Marekani na washirika wake katika hatari ya majibu angamizi ya Iran.
(last modified 2026-08-09T02:57:48+00:00 )
Aug 09, 2026 02:54 UTC
  • Jenerali Daniel Caine, Mkuu wa Majeshi ya Marekani,
    Jenerali Daniel Caine, Mkuu wa Majeshi ya Marekani,

Mkuu wa Majeshi ya Marekani, Jenerali Daniel Caine, amewasihi maafisa wakuu wa utawala wa Trump kutafuta njia ya kupunguza vita na Iran, akionya kwamba ongezeko zaidi la mapigano ya kijeshi haliwezi kupata mafanikio makubwa na kwamba linawaweka wanajeshi wa Marekani na washirika wake katika hatari ya majibu angamizi ya Iran.

CNN imeripoti ikiwanukuu watu watatu waliokuwa karibu na majadiliano hayo, kwamba Caine alielezea wasiwasi wake kwa Mkurugenzi wa CIA John Ratcliffe, Waziri wa Mambo ya Nje Marco Rubio, na Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance Ijumaa iliyopita.

"Caine anatafuta njia ya kujiondoa vitani," chanzo kimoja kimefichua huku maafisa wakuu wakizidi kuhoji kama Rais Donald Trump anaweza kuilazimisha Tehran kukubali matakwa yake.

Ripoti hiyo imesema Jenerali Daniel Caine na maafisa wengine wakuu wa jeshi walikuwa na shaka kuhusu ongezeko la mashambulizi ya kijeshi lililopendekezwa mwishoni mwa Julai kwa sababu ya hofu kwamba Iran inaweza kulipiza kisasi dhidi ya washirika wa Marekani na miundombinu ya nishati ya kikanda.

Maafisa wa Marekani pia wana wasiwasi zaidi kuhusu kupungua kwa akiba ya makombora ya ulinzi wa anga na zana nyingine za kivita, jambo ambalo linaweza kupunguza uwezo wa Washington wa kuendeleza vita vya muda mrefu dhidi ya Iran.

Ripoti hiyo imesema maafisa wa serikali ya Marekani sasa wanatafuta matokeo ambayo Trump anaweza kuyawasilisha kama ushindi wa kisiasa na kuacha wazi mlango kwa diplomasia, ikiwa ni pamoja na makubaliano yanayowezekana ya kufungua tena Lango-Bahari la Hormuz.

Iran ilifunga Lango-Bahari la Hormuz, njia muhimu ya usafirishaji wa nishati duniani, ili kukabiliana na mashambulizi ya kinyama ya Marekani, na kuongeza mashinikizo kwa Washington na washirika wake wa kikanda.