Mwanzilishi mwenza aonya: Wikipedia imekuwa chombo cha propaganda cha CIA, taasisi zingine zenye nguvu
-
Lawrence Mark Sanger
Mwanzilishi mwenza wa Wikipedia, Lawrence Mark Sanger, ameonya kwamba ensaiklopidia hiyo ya mtandaoni imekuwa chombo cha propaganda, akisema Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) na marekebisho yanayofanywa na makampuni mbalimbali kwenye Wikipedia yamedhoofisha sera yake ya kutopendelea upande wowote.
"Wikipedia ilitambuliwa mapema kama chombo muhimu cha propaganda," amesema Sanger katika mahojiano na gazeti la Ujerumani la Berliner Zeitung.
Ameongeza kwa kusema: "Ukweli tunaoujua ni kwamba, kwa mujibu wa ushahidi wa kila aina, CIA tayari imeifanyia mabadiliko Wikipedia."
Ameashiria zaidi ripoti zilizotolewa na Ofisi ya Uandishi wa Habari za Uchunguzi (BIJ), ambayo iligundua kuwa kampuni ya mawasiliano ya Portland Communications ilikuwa imeandika upya maudhui na taarifa zilizoingizwa Wikipedia kwa ajili ya serikali na taasisi tajiri, ikiwa ni pamoja na Qatar, Bill & Melinda Gates Foundation na Libya’s Sovereign Wealth Fund.
Mwanzilishi mwenza wa Wikipedia, Lawrence Mark Sanger ameonya kuwa ushawishi wa Wikipedia sasa umekuwa zaidi ya tovuti kwa sababu injini za utafutaji na roboti za akili mnemba (AI) zinazidi kutumia maudhui yake kwa ajili ya mafunzo.
Sanger pia ameeleza kuwa upashaji habari wa Wikipedia kuhusu mauaji ya kimbari ya Israel huko Gaza umekuwa "wa upendeleo wa waziwazi."
Israel imetumia zaidi ya dola bilioni 1 katika propaganda za kimataifa tangu Oktoba 7, 2023, ikiwa ni pamoja na kampeni zilizoanzishwa kushawishi taarifa zinazopatikana kwa mifumo ya AI.
Sehemu ya pesa hizo zimetolewa kwa kile wataalamu wanachokiita "sumu ya LLM," ambayo ina jukumu la kuanzisha tovuti zinazoiunga mkono Israel zinatoa maelezo na taarifa zilizoidhinishwa na Israel kwa programu au kiolesura cha wavuti (chatbots) kama vile Claude, ChatGPT na Grok wakati watumiaji wanapouliza kuhusu mauaji ya kimbari.