Maandamano Ujerumani na Korea Kusini kupinga utawala wa Kizayuni na kuunga mkono wananchi wa Palestina
Maandamano makubwa yamefanyika nchini Ujerumani na Korea Kusini kupinga sera na vitendo vya kikatili vya utawala wa Kizayuni na kuonyesha mshikamano na wananchi wa Palestina.
Waandamanaji hao wakiwa wamebeba mabango na maberamu wameonyesha uungaji mkono wao kwa Palestina na kupinga kile walichokitaja kuwa ni ukaliaji mabavu wa ardhi za Palestina. Katika maandamano hayo, baadhi ya washiriki walitoa wito wa kukombolewa Palestina.
Waandamanaji katika mji mkuu wa Ujerumani, Berlin, wamefanya maandamano kupinga uungaji mkono wa kijeshi unaotolewa na nchi za Magharibi kwa utawala wa Kizayuni, huku wakitoa kauli za mshikamano na wananchi wa Palestina.
Aidha, mjini Seoul, mji mkuu wa Korea Kusini, wakazi wa mji huo wamefanya maandamano ya kuonyesha mshikamano wao na wananchi wa Palestina, wakitaka kusitishwa uhalifu wa utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza.
Waandamanaji hao walipaza sauti wakisema, “Palestina lazima iwe huru,” huku wakipinga kile walichokitaja kuwa ni ukaliaji mabavu wa maeneo ya Palestina unaofanywa na utawala wa Kizayuni.
Maandamano ya kuunga mkono Palestina na kupinga sera na hatua za Israel yameendelea kufanyika katika miji mbalimbali barani Ulaya.
Katika siku za hivi karibuni, maandamano yamefanyika katika nchi mbalimbali, huku waandamanaji wakitaka kusitishwa mashambulizi ya Israel huko Gaza, kuongezwa misaada ya kibinadamu na nchi za Ulaya kuchukua hatua dhidi ya Israel.
Aidha katika miezi ya hivi karibuni maandamano ya kuunga mkono wananchi wa Palestina yamefanyika pia katika miji mbalimbali nchini Marekani, huku waandamanaji wakitaka kusitishwa mashambulizi katika Ukanda wa Gaza na kuchukuliwa hatua za kuwalinda raia wa Palestina.