"Wanataka kututisha": Mwanachama wa zamani wa Palestine Action akosoa vikwazo vya Trump
https://parstoday.ir/sw/news/world-i141038-wanataka_kututisha_mwanachama_wa_zamani_wa_palestine_action_akosoa_vikwazo_vya_trump
Mwanachama wa zamani wa harakati ya Palestine Action ameikosoa serikali ya Rais Donald Trump wa Marekani kwa kuliwekea vikwazo shirika hilo, ambalo linafanya kazi kwa bidii kupinga biashara ya silaha inayounga mkono mashambulizi ya kijeshi ya Israel dhidi ya watu wa Palestina.
(last modified 2026-08-29T02:46:05+00:00 )
Aug 29, 2026 02:44 UTC

Mwanachama wa zamani wa harakati ya Palestine Action ameikosoa serikali ya Rais Donald Trump wa Marekani kwa kuliwekea vikwazo shirika hilo, ambalo linafanya kazi kwa bidii kupinga biashara ya silaha inayounga mkono mashambulizi ya kijeshi ya Israel dhidi ya watu wa Palestina.

The Intercept imeripoti kuwa, mwanaharakati wa amani wa Marekani, Max Geller anayeishi London, amesema: "Mistari myekundu imevukwa; sasa wanawatendea Wamarekani wa kawaida wanaotaka kupinga mauaji ya kimbari kama magaidi."

Ameendelea kusema: "Wanataka kuwatisha watu wasifikirie hata kuunga mkono au kushiriki katika aina hii ya harakati" akisisitiza kwamba suala kuu linalokusudiwa ni kusababisha madhara ya kwa Palestina.

Kwa upande wake, Huda Ammouri, mwanzilishi mwenza wa Palestine Action, ameiambia The Intercept kwamba wanakabiliwa na mashambulizi yasiyo ya kawaida dhidi ya uhuru wa kujieleza na upinzani kutoka kwa nakundi yale yale yanavyofanya mauaji ya kimbari huko Gaza.

Ameongeza kuwa: "Tuko katika kipindi cha kihistoria ambapo ni muhimu sana kuendelea kupinga na kuimarisha harakati zetu, badala ya kurudi nyuma, na kutotegemea taasisi ambazo kimsingi zinadhibitiwa na makundi tunayopigana nayo."

"Palestine Action" ni vuguvugu la Uingereza linalounga mkono Palestina ambalo linafanya kazi ya kusimamisha mahusiano ya Uingereza na Israel, na linapinga biashara ya silaha kwa ajili ya kuunga mkono operesheni za kijeshi za Israel huko Palestina na kutaka kukomesha utawala wa kibaguzi na mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Wapalestina.

Vuguvugu hilo linasema limesababishia hasara ya mamilioni ya dola kwa kampuni kubwa ya silaha ya Israel iliyoko nchini Uingereza, Elbit Systems, na kupelekea kufunga viwanda viwili kati ya 10 vya kampuni hiyo nchini Uingereza. Jambo hilo lilipelekea kukamatwa zaidi ya wanachama 250 wa wanaharakati hiyo ya Palestine Action.