Waziri wa Fedha wa Ujerumani amwambia Trump: Komesha vita 'visivyo na uwajibikaji' dhidi ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/world-i141052-waziri_wa_fedha_wa_ujerumani_amwambia_trump_komesha_vita_'visivyo_na_uwajibikaji'_dhidi_ya_iran
Waziri wa Fedha wa Ujerumani amemtaka Rais Donald Trump wa Marekani kukomesha vita "visivyo vya kuwajibika" dhidi ya Iran.
(last modified 2026-08-29T10:18:30+00:00 )
Aug 29, 2026 10:14 UTC
  • Lars Klingbeil
    Lars Klingbeil

Waziri wa Fedha wa Ujerumani amemtaka Rais Donald Trump wa Marekani kukomesha vita "visivyo vya kuwajibika" dhidi ya Iran.

Lars Klingbeil alitoa wito huo jana Ijumaa kwa Rais wa Marekani Donald Trump akimtaka akomeshe vita vyake "visivyo na uwajibikaji" dhidi ya Iran, kabla ya safari yake kwenda Marekani wiki ijayo kwa ajili ya mkutano wa kilele wa G20.

Klingbeil, ambaye pia ni makamu wa Kansela wa Ujerumani, amesema katika mahojiano na mtandao wa televisheni wa ARD kwamba: "Huu ndio ujumbe muhimu zaidi ambao lazima uwasilishwe kwa Marekani: Maliza vita hivi."

Vilevile amemlaumu Donald Trump kwa ongezeko la bei ya mafuta, akisema: "Donald Trump ndiye anayebeba dhima ya vita hivi visivyo vya uwajibikaji ambavyo ameanzisha nchini Iran. Haya ndiyo matokeo tunayohisi katika vituo vya mafuta."

Mawaziri wa fedha kutoka nchi za G20 watakutana Asheville, North Carolina, Jumatatu na Jumanne kujiandaa kwa mkutano wa kilele wa G20 huko Miami baadaye mwaka huu.