New York Times: Jeshi la Wanamaji la Marekani lina hali mbaya; meli nne tu zimevuka Hormuz
https://parstoday.ir/sw/news/world-i141198-new_york_times_jeshi_la_wanamaji_la_marekani_lina_hali_mbaya_meli_nne_tu_zimevuka_hormuz
Gazeti la New York Times limekiri kwamba baada ya Iran kushambulia kituo kikuu cha vifaa vya Jeshi la Wanamaji la Marekani huko Bahrain na kukiharibu kikamilifu, hali hivi sasa imezidi kuwa mbaya kwa jeshi la Marekani kiasi kwamba vituo vingine vya dola hilo pia vinahisi kuwa kwenye hatari za waziwazi na haviwezi kujilinda mbele ya mashambulizi ya Iran.
(last modified 2026-10-14T04:35:26+00:00 )
Sep 04, 2026 10:48 UTC
  • New York Times: Jeshi la Wanamaji la Marekani lina hali mbaya; meli nne tu zimevuka Hormuz

Gazeti la New York Times limekiri kwamba baada ya Iran kushambulia kituo kikuu cha vifaa vya Jeshi la Wanamaji la Marekani huko Bahrain na kukiharibu kikamilifu, hali hivi sasa imezidi kuwa mbaya kwa jeshi la Marekani kiasi kwamba vituo vingine vya dola hilo pia vinahisi kuwa kwenye hatari za waziwazi na haviwezi kujilinda mbele ya mashambulizi ya Iran.

Televisheni ya Al-Manar imelinukuu gazeti la Marekani la "The New York Times" likikiri katika ripoti yake kwamba Jeshi la Wanamaji la nchi hiyo limekumbwa na mgogoro mkubwa wa vifaa Mashariki ya Kati.

Kwa mujibu wa New York Times, takriban meli 20 za Marekani zenye karibu wanajeshi wa majini 20,000 na askari wa miguu, zinahitaji zaidi ya milo 420,000 na takriban galoni milioni nane za mafuta kwa wiki.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa, baada ya Iran kuangamiza kikamilifu kituo kikuu cha vifaa cha Jeshi la Wanamaji la Marekani huko Bahrain, hali imezidi kuwa mbaya na kusababisha bandari nyingine zilizoko karibu na kituo hicho kuogopa mno kwa kiwango ambacho zimeamua kusitisha huduma. 

Gazeti hilo la Marekani limeongeza kuwa meli za misaada sasa zinapaswa kusafiri kama maili 2,200 kufikia Kisiwa cha Diego Garcia au hata masafa marefu zaidi ya hayo ili kuweza kufika Singapore.

Huku hayo yakiripotiwa, takwimu zilizochapishwa na makampuni ya meli zinaonesha kuwa, ni meli nne tu za mafuta zilizopita kwenye Lango-Bahari la Hormuz jana Alkhamisi, na safari za meli kwenye lango-bahari hilo imepungua sana katika siku 10 zilizopita.

Shirika la habari la Mehr limeinukuu Al-Hadath ikisema kuwa, takwimu iliyochapishwa na makampuni ya meli inaonesha kuwa ni meli nne tu za mafuta zilizopita kwenye Lango-Bahari la Hormuz jana Alkhamisi.

Makampuni hayo yamethibitisha kwa takwimu sahihi kwamba, idadi ya meli za mafuta zinazopita kwenye Lango-Bahari wa Hormuz imepungua katika siku 10 zilizopita.

Takwimu za makampuni hayo ya meli zimetolewa hukuhuku kampuni ya Kepler, ambayo ina jukumu la kufuatilia safari za meli, kabla ya hapo ilikuwa imetangaza kwamba ni meli sita tu za mizigo zilizopita kwenye Lango-Bahari la Hormuz Jumatano iliyopita, na miongoni mwa meli zilizopita sku hiyo kulikuwa na meli mbili kubwa za kubeba gesi.

Yote hayo yanathibitisha uongo wa madai ya rais wa Marekani, Donald Trump anayedai kwamba eti wao ndio wanaolidhibiti Lango-Bahari la Hormuz hivi sasa.