Rais wa Russia aliamuru jeshi lisitishe mashambulizi dhidi ya Ukraine kwa muda wa siku tatu
Rais Vladimir Putin wa Russia ameamuru kusitishwa mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Ukraine kwa muda wa siku tatu kabla ya mazungumzo na wapatanishi wakuu wa Marekani Steve Witkoff na Jared Kushner, ambao waliwasili mjini Moscow mapema leo Jumamosi.
Mazungumzo hayo yanatarajiwa kuzingatia njia za kutatua mgogoro wa Ukraine. Witkoff na Kushner wanatarajiwa kutembelea Kiev pia baada ya mikutano yao ya Moscow, ambayo inajumuisha mazungumzo watakayofanya na Putin.
Akizungumza mapema leo, msemaji wa Ikulu ya Russia, Kremlin, Dmitry Peskov alisema: "Rais wa Russia [na] Amiri Jeshi Mkuu Putin ameamuru [vikosi vya jeshi] visifanye mashambulio dhidi ya Kiev kwa muda wa siku tatu kuanzia saa sita usiku wa leo."
Peskov ameongeza kuwa uamuzi huo unakusudiwa kuwaruhusu Witkoff na Kushner kufanya mazungumzo na maafisa wa Ukraine katika mji mkuu wa nchi hiyo.
Vyombo kadhaa vya habari vya Ukraine viliripoti mapema leo kwamba vikosi vya Kiev navyo pia vilikuwa vimeagizwa kusimamisha mashambulizi kuanzia saa sita usiku Jumamosi hadi Jumanne…/