May 29, 2023 01:31 UTC
  • Mamia ya athari za kale za Afghanistan zilizoibiwa wakati wa uvamizi wa Marekani zarejshwa nchini + Video

Mamia ya vipande vya athari za kale zilizoibiwa wakati wa uvamizi na vita vilivyoanzishwa na wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan vimerejeshwa kwenye jumba la makumbusho la nchi hiyo.

 

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB, Yahya Mohibzadeh, Naibu Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Afghanistan, amesema: "mwaka jana, ulizuiliwa utoroshaji wa vipande 1,000 vya athari za sanaa za kihistoria; na athari kadhaa za kale zilirejeshwa kwenye Jumba la Makumbusho ya Taifa".

Mohibzadeh ameongeza kuwa, utoroshaji wa athari za kale nchini Afghanistan ulianza tokea muda mrefu nyuma na baadhi ya athari hizo za kale ziliibwa kwenye jumba hilo la makumbusho katika kipindi cha wakati wa vita.

Naibu Mkuu wa Jumba la Makumbusho ya Taifa la Afghanistan amedokeza kuwa, miongo kadhaa ya mapigano na vita imeiangamiza Afghanistan, na wahalifu na wasafirshaji vitu kimagendo waliitumia fursa hiyo ya kukosekana amani na uthabiti nchini kupora athari za kihistoria kwenye majengo na maeneo ya kihistoria na ya kale.../

Tags