Machapisho yaliyochaguliwa ya watumiaji wa X; Kutoka salamu za ghera kwa mwanamke wa Kiirani hadi kukosoa ushirikiano wa Magharibi na utawala wa Kizayuni.
https://parstoday.ir/sw/radio/iran-i127338-machapisho_yaliyochaguliwa_ya_watumiaji_wa_x_kutoka_salamu_za_ghera_kwa_mwanamke_wa_kiirani_hadi_kukosoa_ushirikiano_wa_magharibi_na_utawala_wa_kizayuni.
Watumiaji wa mtandao wa kijamii wa "X" wametoa radiamali zao kwa masuala mbalimbali ya kimataifa katika jumbe zao.
(last modified 2026-02-05T12:50:29+00:00 )
Jun 08, 2025 13:00 UTC
  • Machapisho yaliyochaguliwa ya watumiaji wa X; Kutoka salamu za ghera kwa mwanamke wa Kiirani hadi kukosoa ushirikiano wa Magharibi na utawala wa Kizayuni.

Watumiaji wa mtandao wa kijamii wa "X" wametoa radiamali zao kwa masuala mbalimbali ya kimataifa katika jumbe zao.

Jinai za utawala wa Kizayuni wa Gaza, kukamatwa kwa mwanamke wa Kiirani mkosoaji wa Israel huko Ufaransa, na uwongo wa vyombo vya habari vya Magharibi ni miongoni mwa masuala ambayo watumiaji wa mtandao wa kijamii wa "X" walionyesha radiamali, na hilo linajadiliwa katika makala hii kutoka Parstoday.

Kushikiana na wauaji wa watoto

Mtumiaji  wa X aitwaye Alon Mizrahi katika ujumbe wake wa Twitter kwenye mtandao wa kijamii wa X aliashiria uungaji mkono wa nchi za Magharibi kwa utawala wa Kizayuni na kuandika: Balozi zote za Tel Aviv, zikiwemo balozi za Australia, Kanada, Uingereza, Ufaransa, Ugiriki, Italia, Uturuki na nchi nyingine nyingi ziko wazi. Hii ina maana kwamba wanaidhinisha na wanashiriki katika kile ambacho Israel imefanya kwa watoto wa Kipalestina.

Salamu na ghera kwa bibie wa Iran

Mtumiaji X wa mtandao wa kijamii "Mohsen Maghsoudi" alikosoa kukamatwa kwa raia wa Iran Mahdia Esfandiari na polisi wa Ufaransa klatika ujumbe wake. Aliandika: Laana ziwe juu ya kauli mbiu yenu ya haki za binadamu, salamu kwa ghera ya mwanamke huyu msomi wa Kiirani anayeishi Ufaransa, ambaye amefungwa katika kitovu cha haki za binadamu na uhuru wa kujieleza kwa kosa la kukosoa jinai dhidi ya Gaza na kulaani mauaji ya halaiki.

Ubaya kupita maneno

Hamza Yusuf, mtumiaji mwingine wa mtandao wa kijamii wa X, aliona uhalifu wa Israel huko Gaza kuwa uovu kupita maneno. Aliandika: mzingiro wa kutwisha; kuwabakisha na njaa watu wote na kusababisha njaa. Kisha waliwarubuni kwa ahadi za chakula na msaada, lakini mwishowe wakawaua.

Uwongo wa vyombo vya habari vya Magharibi

Katika ujumbe wake, mtumiaji wa mtandao wa kijamii wa X anayeitwa Tucker Carlson amezunguumzia hadaa na udanganyifu wa vyombo vya habari vya Magharibi. Aliandika: CNN ilidanganya kuhusu matatizo ya akili ya Joe Biden kwa miaka mitano, ikavuja, na kisha badala ya kuomba msamaha, ikajifanya kufichua hadithi ya kuharibika kwa ubongo wa Biden. Ndiyo maana kila mtu mwaminifu duniani anachukia vyombo hivi vya habari.

Mpango wa Uwongo

Mtumiaji mwingine anayeitwa Ramzy Baroud alizingatia mpango wa Marekani wa kuanzisha usitishaji vita huko Gaza kama mpango wa ulaghai. Aliandika: Usidanganywe na mapendekezo yaliyoundwa kwa madhumuni ya kisiasa. Mpango wa Witkoff unampa Netanyahu njia ya maisha na Trump ushindi katika sera ya kigeni wakati Wapalestina wanakabiliwa na uharibifu unaoendelea. Hatuwezi kukubali kifo cha taratibu. Madai ya Wapalestina hayayumbishwi: Kukomeshwa vita, hakikisho la msaada kamili na mafuta, na ujenzi mpya wa Gaza.