"Dunia bila Israeli ni mahali pazuri zaidi kwa watoto"; radiamali ya watumiaji X kwa kilio cha mtoto wa Kipalestina katika shule iliyolipuliwa huko Gaza
Msichana wa Kipalestina aliokolewa kimiujiza katika shule moja kwenye Ukanda wa Gaza ambayo ilikuwa ikiteketea kabisa na moto na vilio vya wanawake na watoto vilisikika.
Shule ya Fahmi al-Jarjawi iliyoko katika kitongoji cha al-Darj katika mji wa Gaza, iliyokuwa ikitumika kama makazi ya wakimbizi wa Kipalestina, ilishambuliwa kwa bomu katika mashambulizi ya anga ya utawala wa Kizayuni usiku wa kuamkia jana.
Kulingana na Pars Today, kufuatia shambulio hilo, jengo la shule hiyo liliporomoka na moto mkubwa ukazuka ndani yake, na kuua makumi ya wanawake na watoto. Vilio vyao na maombi yao ya kuomba msaada yalisikika katikati ya moto. Uhalifu na jinai hii ilikuwa na radiamali nyingi kati ya watumiaji wa mtandao wa kijamii wa X.
Wamewachoma moto hai watoto wa Kipalestina
Seyed Mohammad Marandi, profesa wa chuo kikuu na mchambuzi wa masuala ya kisiasa aliandika kwenye mtandao wa kijamii wa X: Uingereza inausaidia utawala wa Kizayuni kuwachoma moto watoto wa Gaza. Marandi aliandika kwenye ujumbe mwingine: Gaza iko wapi? Ni mahaa ambapo watoto wa Kipalestina walichomwa moto wakiwa hai?
Dunia bila Israeli ni mahali pazuri zaidi kwa watoto
Mtumiaji mwingine aitwaye Salahuddin aliandika kwenye mtandao wa kijamii wa X: Hii ni hadithi ya kila siku ya watoto huko Gaza ... ulimwengu bila Israeli ni mahali pazuri zaidi kwa watoto ...
Mtoto wa Kipalestina katikati ya moto: Haya ni mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni
Hossein Yazdi aliandika kwenye mtandao wa kijamii: Mtoto wa Kipalestina akijaribu kutoroka kutoka ndani ya moto, picha hii ilipigwa katika shule ya Fahmi al-Jarjawi katika Jiji la Gaza, ambayo ni makazi ya familia za Wapalestina waliofurushwa. Shule hii ilishambuliwa na Israel; haya ni mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni na uungaji mkono wa nchi za Magharibi.
Watoto wa Gaza; Kichwa cha habari cha kwanza cha mashirika ya habari duniani
Mohammad Safa, mtumiaji wa mtandao wa kijamii wa X, aliandika: Video ya mtoto huyo wa Kipalestina akirandaranda kati ya moshi na moto inapaswa kuwa katika ukurasa wa mbele wa mashirika yote ya habari duniani. Msichana wa Kipalestina akijaribu kutoroka moto baada ya shule yake kushambuliwa kwa bomu alipokuwa amelala.
Watoto wa Gaza, watoto wasio na hatia katika ardhi ya vita
Mtumiaji mwingine aitwaye Mahdi aliandika katika mtandao wa kijamii wa X kwa muuundo wa shairi kwa ajili ya watoto wa Gaza: Watoto wa Gaza, watoto wasio na hatia katika ardhi ya vita, chini ya mzigo wa mateso na hatia, tabasamu zao zimefungwa kwenye kona ya giza, macho yao yamejaa maumivu na chuki ya muda mrefu, anga yao imejaa moshi na moto, mchezo wao umeachwa kwenye kona ya dunia, lakini macho ya walimwengu yamefungwa, watoto wa Gaza wasio na sauti wanapaza sauti.