Seyyed Abbas Araghchi: Iran inalaani jaribio lolote la kudhuru umoja wa Waislamu
May 28, 2025 04:07 UTC
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: Tehran inalaani vikali jaribio lolote la kushambulia umoja wa Waislamu.
Seyed Abbas Araghchi, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran Jumanne aliandika kwenye akaunti ya X: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inalaani vikali jaribio lolote la kudhuru umoja wa Waislamu hususan katika anga ya kiroho ya Hija. Tumeazimia kutoruhusu mtu yeyote kuharibu uhusiano wetu wa kindugu na majirani zetu, pamoja na hatua nzuri zilizopigwa katika uhusiano na Saudi Arabia.
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran ameongeza kuwa: Iran inathamini usimamizi mzuri na unaofaa wa Hija ya mwaka huu.
Tags