Dec 31, 2022 08:22 UTC
  • Hamasa ya tarehe 9 Dei; Siku ya Ung'amuzi na Muono wa Mbali

Tarehe 9 Dei mwaka 1388 Hijria Shamsia iliyosadifiana na tarehe 30 Disemba 2009, mamilioni ya wananchi wa Tehran na miji mingine hapa nchini walifanya maandamano makubwa kulalamikia machafuko ya barabarani na himaya ya madola ya Magharibi kwa machafuko hayo.

Maandamano haya yamekuwa tukio lililobakia katika historia ya Mapinduzi ya Kiislamu.  Mwaka 1388 Hijria Shamshia (2009) kulifanyika uchaguzi kama zilivyokuwa chaguzi za hapo kabla hapa Iran. Ushiriki wa asilimia 85 wa wananchi katika uchaguzi wa rais wa duru ya kumi ilikuwa ni ishara ya wazi ya kuendelea kigezo cha mfumo wa demokrasia ya Kiislamu yenye ridhaa ya wananchi hapa Iran.

Mahdi Fazaeli, mtaalamu wa masuala ya kisisa sambamba na kubainisha nukta hii kwamba, taifa hili lilitwishwa gharama ya harakati na njama hii amesema kuwa, moja ya sababu za kuwa tata fitina ya mwaka 2009 ni kwamba, kundi lililo dhidi ya mapinduzi lilitumia suhula zote katika kipindi hicho. Suhula na uwezo huo hawakuuingiza katika uchaguzi tu, bali lengo lao kuu lilikuwa ni kuuangusha mfumo wa Kiislamu hapa nchini. Ukweli wa mambo ni kuwa, lengo la Marekani katika fitina ya 1388 (2009) lilijengeka katika msingi wa ‘kupiga ndege wawili kwa jiwe moja’.

Wapangaji wa fitina hii kwa upande mmoja walilenga asili na usahihi wa uchaguzi na katika upande mwingine walikuwa na ndoto za kutekeleza mapinduzi laini. Ni kutokana na sababu hiyo ndio maana machafuko ya barabarani yaliyoibuka baada ya uchaguzi wa rais wa duru ya kumi mwaka huo halikuwa tukio la kawaida, bali ni tukio lililokuwa na kigezo cha mapinduzi laini au mapinduzi ambayo ni mashuhuri kwa jina la ‘mapinduzi ya mahameli’.

 

Ushahidi na nyaraka zilizopatikana baada ya fitina hiyo zinaonyesha kuwa, vibaraka kutoka nje hususan waliotumwa na Marekani na baadhi ya madola ya Ulaya walikuwa viongozi wa njama hii.

Saadullah Zarei, mtaalamu wa masuala ya kimataifa katika kutoa tathmini yake kuhusiana na sababu zilizokuwa na taathira katika fitina ya 1388 (2009) anaashiria nafasi na mchango wa vyombo vya habari na uingiliaji wa baadhi ya viongozi wa Marekani na Ulaya katika kuwaunga mkono wasimamiaji na watekelezaji wa fitina hiyo na kusema: Njama hii kama ilivyokuwa katika kipindi cha miaka minane ya vita vya kulazimishwa Iran na Iraq ambapo wahusika walishirikiana na adui na wakawa kambi za vikosi vya Iraq, katika tukio la fitina ya 2009 walijitokeza pia uwanjani na wakatoa himaya na uungaji mkono wao.

 

Hata hivyo ni jambo lililo wazi ni kwamba, katika kuundika fitina hii, mtindo na mbinu isiyo sahihi ya baadhi ya wagombea wa uchaguzi huo wakati wa midahalo ya uchaguzi ilikuwa sababu ya uchaguzi huo kuingia katika utata na upande hatari. Katika uwanja huo harakati isiyo ya kawaida iliyofanywa na makundi yanayotafuta fursa kwa kisingizio cha kumuunga mkono mgombea aliyeshindwa, yalijitokeza na kuvunjia heshima thamani na nembo za Ashura katika maombolezo ya mwezi wa Muharram na kuvaa vazi la harakati iliyo dhidi ya dini.

Hata hivyo katika tarehe 9 Dei yaani katika siku kama ya leo miaka 11 iliyopita, mamilioni ya wananchi wa Tehran na miji mingine hapa nchini walifanya maandamano kulalamikia machafuko ya barabarani na himaya ya madola ya Magharibi kwa machafuko hayo. Kama alivyoseئa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ni kuwa, tukio hilo lilikuwa moja ya vilele visivyoweza kusahaulika katika ushindi ambapo kwa ung’amuzi na muono wa mbali na kwa kusoma alama za nyakati, wananchi wa Iran waliweza kuishinda anga iliyokuwa imetiwa vumbi ambapo kwa kutegemea imani na irada ya Mwenyezi Mungu, wakaweza kusajili katika histroria ya Mapinduzi ya Kiislamu siku ambayo katu haiwezi kusahaulika.

 

Katika moja ya miongozo yake, Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu anaashiria njama mtawalia za Marekani zenye lengo la kuzusha utata na kuwapokonya wanachi wa Iran matumaini na hali ya kujiamini ya kitaifa na kusema kuwa: Tarehe 9 Dei kwa adhama yake, ilikuwa siku ya jibu la wananchi kwa mchezo kama huu na kutetea thamani za mapinduzi na dini, ambapo hii leo pia tabaani kungali kuna mjadala wa kudumu na kubakia thamani za dini na Mapinduzi ya Kiislamu.

Kwa msingio huo basi, inapaswa kutathmini hamasa ya tarehe 9 Dei katika kipimo cha kuchukua kasi Harakati ya Mwamko wa Mapinduzi. Hatua ya wananchi wa Iran ya kuhudhuria katika maandamano makubwa ya tarehe 9 Dei wakiwa na ung’amuzi na muono wa mbali maandamano ambayo yalifanyika katika mhimili wa umoja na kutii Wilaya (uongozi), ilionyesha kiwango chao cha hali ya juu cha kumtambua adui na kudhihirisha hilo mkabala na harakati za upotofu. Siku hii ya tarehe 9 Dei imepewa jina la "Siku ya Ung'amuzi na Muono wa Mbali”.

Tags