-
AU, ECOWAS zalaani jaribio la mapinduzi Benin; zasema zinaiunga mkono serikali
Dec 07, 2025 23:37Umoja wa Afrika (AU) na Jumuiya ya Uchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) zimelaani jaribio la mapinduzi nchini Benin siku ya Jumapili, na kueleza kuwa zinaiunga mkono serikali katika kudumisha utaratibu wa kikatiba.
-
AU yalaani shambulio la RSF lililoua zaidi ya raia 100 katika mji wa Kalogi, kusini mwa Sudan
Dec 07, 2025 23:05Umoja wa Afrika, AU umelaani vikali mashambulizi ya ndege zisizo na rubani yaliyofanywa na Vikosi vya Usaidizi wa Haraka, RSF yaliyoua makumi ya watu wakiwemo watoto katika mji wa Kalogi kusini mwa Sudan.
-
Mgombea urais Uganda: Nilipigwa na askari usalama
Dec 07, 2025 08:49Bob Wine au Robert Kyagulanya mgombea kiti cha urais nchini Uganda kwa tiketi ya chama cha upinzani cha NUP amesema kuwa askari usalama wa nchi hiyo wampiga yeye na wafuasi wake wakati walipokuwa katika kampeni za uchaguzi kaskazini mwa nchi hiyo katika kile kinachotajwa kuwa muendelezo wa ghasia na utumiaji mabavu unaoshuhudiwa Uganda kabla ya uchaguzi wa Rais Januari 15 mwakani.
-
Vikosi vya serikali ya Benin vyazima jaribio la mapinduzi, waziri asema hali 'imedhibitiwa'
Dec 07, 2025 08:16Vikosi vya usalama vya Benin vimezima jaribio la mapinduzi, huku hali ya mambo ikidhibitiwa. Haya yamebainishwa na Waziri wa Fedha Romuald Wadagni alipohojiwa na jarida la Jeune Afrique hii leo.
-
Madaktari wa Sudan: Tumesajili kubakwa wanawake 19 na RSF huko El Fasher
Dec 07, 2025 07:51Mtandao wa Madaktari wa Sudan umetangaza kuwa timu zake katika kambi ya Al-Afad, mashariki mwa mji wa Al-Dabba kaskazini mwa Sudan, zimesajili visa 19 vya ubakaji wa wanawake waliofurushwa kutoka El-Fashir hadi katika mji wa Al-Dabba na wanachama wa kundi la waasi wa RSF.
-
Mamia waandamana Mogadishu kumlaani Trump kwa kuwatukana Wasomali
Dec 06, 2025 22:53Mamia ya watu wamemiminika mitaani huko Mogadishu mji mkuu wa Somalia kuonesha hasira zao dhidi ya rais wa Marekani Donald Trump aliyewatukana Wasomali na kuwaita "takataka."
-
Sudan yawatuhumu wanamgambo wa RSF kwa kuuwa raia 79 huko Kordofan Kusini
Dec 06, 2025 10:02Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan imewatuhumu wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) kuwa wameua raia 79 wakiwemo watoto 43 katika mauaji ya halaiki kwenye mji wa Kalogi katika jimbo la Kordofan Kusini.
-
Wakimbizi wa Burundi watakiwa kuondoka Tanzania
Dec 06, 2025 04:20Serikali ya Tanzania imetangaza rasmi kufuta hadhi ya ukimbizi na kuzifunga kambi za wakimbizi wa Burundi waishio mkoani kigoma kabla ya mwezi Juni mwaka ujao wa 2026.
-
Mapigano yaendelea mashariki mwa DRC licha ya Kagame na Tshisekedi kusaini makubaliano ya amani
Dec 06, 2025 04:19Mapigano makali yameendelea kushuhuudiwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo siku moja baada ya marais wa nchi hiyo kusaini makubaliano mapya ya amani mjini Washington Marekani.
-
AfDB yatoa msamaha wa karibu dola milioni 18 za kwa Somalia
Dec 05, 2025 23:11Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imesema kuwa, imeidhinisha kusamehewa Somalia karibu dola milioni 18 na hivyo kufungua njia ya kufutwa kabisa mikopo yote ya nchi hiyo ambayo inajumuisha ya kipindi cha baina ya mwaka 2024 hadi 2039.