-
Je, kwa nini Ujerumani, muungaji mkono mkubwa zaidi wa Ulaya kwa utawala wa Kizayuni, sasa inaonekana kuukosoa utawala huo?
May 29, 2025 06:18Friedrich Mertz, Kansela wa Ujerumani alibadilisha sauti yake kuhusiana na utawala wa Kizayuni mnamo Jumanne, Mei 27 na kusema: "Mashambulio makubwa ya kijeshi ya Waisraeli katika Ukanda wa Gaza hayana mantiki tena kwangu."
-
Onyo la Trump kwa Netanyahu baada ya kutishia kuishambulia Iran
May 29, 2025 06:17Rais wa Marekani, Donald Trump ameripotiwa kuvutana na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu katika mazungumzo yao ya simu, baada ya nduli huyo wa vita wa utawala wa Kizayuni kutishia kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran, na hivyo kuhatarisha mazungumzo ya kidiplomasia yanayoendelea kati ya Tehran na Washington.
-
Russia yajibu baada ya Trump 'kumtishia nyau' Putin eti 'anacheza na moto'
May 28, 2025 06:48Rais wa Marekani, Donald Trump ametoa matamshi ambayo yanaonekana ya kumtishia mwenzake wa Russia, Vladimir Putin, ambapo amesema "anacheza na moto," bila kufafanua nini hasa anamaanisha.
-
Mauaji Gaza; Majaji, mawakili 800 wa UK wataka Israel ifukuzwe UN
May 28, 2025 06:47Kundi la mawakili waandamizi, majaji wa zamani na wasomi wengine zaidi ya 800 wa Uingereza wameitaka serikali ya London kuuwekea vikwazo utawala wa Israel, na kushinikiza kusimamishwa uanachama wa Tel Aviv katika Umoja wa Mataifa.
-
Je, kwa nini uadilifu wa rangi ni nara tupu isiyotekelezeka huko Marekani?
May 28, 2025 06:02Miaka mitano baada ya kuuawa kikatili George Floyd, kijana Mmarekani mweusi, na polisi wa nchi hiyo, hatua na sera zilizoahidiwa kutekelezwa na serikali ya Marekani na makampuni mengi makubwa ya kiuchumi nchini humo kwa ajili ya hakikisha haki na usawa vinadumishwa kati ya jamii na watu wa rangi tofauti wa nchi hiyo zimesahaulika kabisa.
-
Ubelgiji: Ni mambo gani mengine ya kutisha lazima yatokee Gaza hata tuyaite ni mauaji ya kimbari?
May 28, 2025 02:09Waziri wa Mambo ya Nje wa Ubelgiji Maxime Prévot ameulaumu vikali Umoja wa Ulaya kuhusu mauaji ya kimbari ya Israel huko Gaza, akisema hali ya sasa imevuka ghadhabu ya kimaadili na sasa inahitaji hatua madhubuti za adhabu.
-
Mataifa masikini yakabiliwa na wimbi la madeni ya China
May 28, 2025 02:07Mataifa masikini duniani sasa yanakabiliwa na wimbi kuubwa la madeni ya China na kuyaweka katika hali mbaya kutokana na kulemewa na madeni hayo.
-
Radiamali za kindumakuwili kwa jinai za Israel; kuanzia maandamano ya wananchi hadi kimya cha serikali
May 28, 2025 02:07Wiki ya mwisho ya mwezi Mei 2025 imekuwa nukta ya kuanzia mabadiliko katika mchakato wa kueneza hasira za walimwengu dhidi ya jinai za utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza.
-
Balozi wa Colombia: Dunia isifumbie macho mateso ya watu wa Gaza
May 27, 2025 06:38Jorge Ivan Ospina, balozi mpya wa Colombia katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu amesema "ulimwengu haupaswi kuwafumbia macho" raia wa Palestina wanaoteseka huko Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan unaokaliwa kwa mabavu.
-
Mataifa ya Kiislamu yatakiwa yaungane kukabiliana na 'Islamophobia'
May 27, 2025 06:33Rais wa Azerbaijan, Ilham Aliyev ametoa wito kwa mataifa ya Kiislamu kuungana na kusimama bega kwa bega katika kupambana na chuki dhidi ya Uislamu.