Araqchi: Trump amesaliti diplomasia na watu wa Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i137156-araqchi_trump_amesaliti_diplomasia_na_watu_wa_marekani
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran amesema kuwa Rais wa Marekani, Donald Trump ameisaliti diplomasia na watu wa Marekani waliompigia kura akisisitiza kuwa: Wakati uongo mkubwa unapopotosha ukweli wa mambo, maratajio yasiyo ya kweli katu hayawezi kutimizwa.
(last modified 2026-03-04T12:06:42+00:00 )
Mar 04, 2026 12:06 UTC
  • Sayyid Araqchi
    Sayyid Araqchi

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran amesema kuwa Rais wa Marekani, Donald Trump ameisaliti diplomasia na watu wa Marekani waliompigia kura akisisitiza kuwa: Wakati uongo mkubwa unapopotosha ukweli wa mambo, maratajio yasiyo ya kweli katu hayawezi kutimizwa.

Sayyid Abbas Araqchi ameyasema hayo katika ujumbe uliotumwa kwenye mtandao wa kijamii wa X. Ameashiria mienendo ya Donald Trump kuhusu mwenendo wa diplomasia ulioanza kati ya Marekani na Iran na kusema: Wakati mazungumzo magumu ya nyuklia yanapofanywa kama muamala wa kuuza na kununua milki, na pindi uongo mkubwa unapotumiwa kupotosha ukweli, matarajio yasiyo halisi kamwe hayawezi kutimia. Matokeo yake ni kupigwa mabomu meza ya mazungumzo kwa chuki na inda.

Donald Trump

Sayyid Araqchi amesisitiza kuwa Trump ameisaliti diplomasia na pia Wamarekani waliompigia kura. 

Jumamosi ya tarehe 28 Februari Marekani na utawala haramu wa Israel zilianzisha mashambulizi dhidi ya ardhi ya Iran na kumuua shahidi Kiongozi Mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu pamoja na makamanda kadhaa wa ngazi za juu wa jeshi, wakati Iran na Marekani zikiwa zimekamilisha duru tatu za mazungumzo ya nyuklia na zikijitayarisha kwa duru ya nne ya mazungumzo hayo.