-
Majeshi ya Iran: Tumejiandaa kutoa pigo kali kwa uchokozi wowote wa adui
Dec 30, 2025 10:45Vikosi vya Ulinzi vya Iran vimetangaza kuwa, vimejiandaa kikamilifu kutoa majibu makali kwa tishio lolote la usalama wa Jamhuri ya Kiislamu na watu wake na kuonya kwamba, uchokozi wowote mpya wa uadui dhidi ya Iran utakuwa mkali zaidi, angamizi zaidi na wenye madhara makubwa zaidi kuliko huko nyuma.
-
Iran yaonya: Israel inalenga kudhoofisha uthabiti kwa kutambua 'Somaliland' kama nchi huru
Dec 30, 2025 06:37Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imepinga kwa mara nyingine hatua ya utawala wa Kizayuni kutangaza kutambua eneo la Somaliland la Somalia kama nchi huru, ikieleza kuwa sehemu ya mkakati mpana wa kuleta machafuko katika eneo.
-
Iran yajibu vitisho vya Trump, yaapa kwamba 'jibu kali' litatolewa kwa uchokozi wowote
Dec 30, 2025 03:26Admirali Ali Shamkhani, Mshauri mwandamizi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amelaani vikali vitisho vipya vilivyotolewa na Marekani vya kuishambulia kijeshi Jamhuri ya Kiislamu, akiapa kuwa jibu kali litatolewa endapo utafanywa uchokozi wowote ule.
-
Araqchi: Jenerali Soleimani alikuwa 'Mbunifu wa Mhimili wa Muqawama' Magharibi mwa Asia
Dec 29, 2025 11:51Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amemsifu shahidi na kamanda wa vita dhidi ya ugaidi, Luteni Jenerali Qassim Soleimani na kumtaja kuwa "mbunifu wa Mhimili wa Muqawama" katika eneo Magharibi mwa Asia.
-
Jeshi la Iran: Tupo katika hali bora zaidi kumkabili adui
Dec 29, 2025 09:53Jeshi la Iran limeonya kwamba, hatua yoyote ya uadui kutoka kwa maadui itakabiliwa na jibu kali, huku likisisitiza juu ya utayarifu wake wa kulilinda na kulihami taifa.
-
Araqchi: Tunaunga mkono mamlaka ya kujitawala na umoja wa ardhi ya Yemen
Dec 29, 2025 07:31Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araqchi amesema kuna ulazima wa kulindwa umoja wa ardhi na mamlaka ya kujitawala ya Yemen, huku kukiwa na ongezeko la mvutano katika maeneo ya kusini mwa nchi hiyo ya Kiarabu.
-
Mawimbi ya kwanza ya satelaiti tatu za Iran yapokewa ardhini kwa mafanikio + VIDEO
Dec 29, 2025 03:21Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wa Iran ametangaza kwamba mawimbi ya kwanza ya satelaiti zote tatu zilizobuniwa na kutengenezwa ndani ya Iran zinazoitwa "Zafar 2", "Paya" na "Kowsar" zilizotumwa angani Jumapili jioni Disemba 28, 2025 yamepokewa kwa mafanikio ardhini akisisitiza kuwa, hii inathibitisha uzima wa kiufundi na utendajikazi mzuri wa satelaiti hizo za Iran baada ya kuingia kwenye obiti.
-
Satelaiti tatu za Iran zarushwa katika anga za mbali, ni hatua madhubuti ya kiteknolojia
Dec 28, 2025 13:01Satelaiti tatu za Iran zilizoundwa ndani ya nchi , ‘Paya’, ‘Zafar 2’ na ‘Kowsar’, leo zimerushwa katika anga za mbali kwa kutumia roketi ya kubeba satelaiti aina ya Soyuz kutoka kituo cha anga cha Vostochny kilichoko nchini Russia.
-
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Qatar wajadili matukio ya kikanda hasa hali ya Yemen
Dec 28, 2025 10:29Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Qatar wamezungumza kwa njia ya simu na kubadilishana mawazo kuhusu matukio ya kikanda hususan matukio ya karibuni huko Yemene. Wamesema kuwa ipo haja ya kulindwa mamlaka ya kujitawal ya ardhi nzima ya nchi hiyo.
-
Iran: Tumejiandaa kutoa jibu chungu zaidi kwa wavamizi
Dec 28, 2025 06:47Rais Masoud Pezeshkian wa Iran ameonya kwamba, kitendo chochote cha uchokozi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu kitakabiliwa na jibu la haraka na la kuumiza zaidi, akisisitiza utayarifu wa Vikosi vya Jeshi vya nchi hii kukabiliana na maadui na vitisho vyao.