Jen. Mousavi: Iran imeivurumishia Israel makombora 30 ya balestiki
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i137358-jen._mousavi_iran_imeivurumishia_israel_makombora_30_ya_balestiki
Kamanda wa Kikosi cha Anga za Mbali cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran IRGC amesema asilimia kubwa ya makombora 30 ya balestiki yaliyovumishwa na Jamhuri ya Kiislamu usiku wa Lailatul Qadr yalipiga shabaha zilizokusudiwa kwa usahihi mkubwa.
(last modified 2026-03-14T03:48:07+00:00 )
Mar 14, 2026 03:48 UTC
  • Jen. Mousavi: Iran imeivurumishia Israel makombora 30 ya balestiki

Kamanda wa Kikosi cha Anga za Mbali cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran IRGC amesema asilimia kubwa ya makombora 30 ya balestiki yaliyovumishwa na Jamhuri ya Kiislamu usiku wa Lailatul Qadr yalipiga shabaha zilizokusudiwa kwa usahihi mkubwa.

Brigedia Jenerali Majid Mousavi amesema makombora hayo ya balestiki yenye uzito wa tani moja hadi mbili ya Iran yalilenga maene yaliyokusudiwa katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na kupachikwa jina bandia la Israel.

Amesema operesheni hizo za Kikosi cha Anga za Mbali cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran IRGC zimeharibu kikamilifu mifumo muhimu ya anga za mbali ya utawala mtenda jinai wa Kizayuni.

Kamanda wa Kikosi cha Anga za Mbali cha Jeshi la IRGC ameeleza bayana kuwa, kufuatia operesheni hizo, sehemu ya anga ya utawala haramu wa Israel ipo wazi na katika hatari ya kushambuliwa muda wowote na Vikosi vya Ulinzi vya Iran.

Operesheni hiyo ya makombora 30 ya balestiki yaliyovumishwa na Jamhuri ya Kiislamu usiku wa Lailatul Qadr inahesabiwa kuwa mashambulizi makubwa zaidi ya kulipiza kisasi ya Jeshi la Iran dhidi ya utawala unaoua watoto wa Israel tangu lianzishe Operesheni ya Ahadi ya Kweli ya 4 mnamo Februari 28.

Itakumbukwa kuwa, Marekani na Israel zilianzisha hujuma za kigaidi dhidi ya Iran Jumamosi ya tarehe 28 Februari na kumuua shahidi  Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, makamanda kadhaa wa kijeshi, na mamia raia wakiwemo watoto wadogo.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesisitiza kuwa itaendeleza mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Operesheni ya Ahadi ya Kweli 4, ili kuwaadhibu vikali maadui walioanzisha uchokozi.