Mkuu wa IRGC: Iran imelipigisha magoti jeshi lenye silaha nyingi zaidi duniani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i140690-mkuu_wa_irgc_iran_imelipigisha_magoti_jeshi_lenye_silaha_nyingi_zaidi_duniani
Mkuu wa Jeshi la Walinzi mwa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) amesema kuwa, Iran imefanikiwa “kulipigisha magoti jeshi lenye silaha nyingi zaidi katika historia ya dunia”, kupitia operesheni za mashambulizi na ulinzi zilizotekelezwa kwa mafanikio licha ya mashambulizi makali ya adui.
(last modified 2026-08-15T11:05:32+00:00 )
Aug 15, 2026 11:00 UTC
  • Mkuu wa IRGC: Iran imelipigisha magoti jeshi lenye silaha nyingi zaidi duniani
    Mkuu wa IRGC: Iran imelipigisha magoti jeshi lenye silaha nyingi zaidi duniani

Mkuu wa Jeshi la Walinzi mwa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) amesema kuwa, Iran imefanikiwa “kulipigisha magoti jeshi lenye silaha nyingi zaidi katika historia ya dunia”, kupitia operesheni za mashambulizi na ulinzi zilizotekelezwa kwa mafanikio licha ya mashambulizi makali ya adui.

Katika ujumbe wake leo, akivishukuru vikosi hivyo kwa miezi sita ya “juhudi za kijihadi ambazo hazijawahi kushuhudiwa,” Meja Jenerali Ahmad Vahidi ameema kuwa, utendaji wao dhidi ya “maadui wakatili zaidi wa wanadamu” umevutia ulimwengu na kufufua matumaini miongoni mwa waliodhulumiwa kwamba, hatimaye wanaweza kuyashinda madola makubwa duniani.

Meja Jenerali Vahidi amesema katika sehemo moja ya ujumbe wake huo: “Ninyi, mkimtegemea Mwenyezi Mungu na kupigana kwa ushindi katika mazingira magumu mno—kuanzia joto kali na unyevunyevu mkubwa katika visiwa na maeneo ya pwani ya kusini, hadi baridi kali katika milima mirefu ya mpakani kaskazini—mlilipigisha magoti jeshi lililo na silaha nyingi zaidi katika historia ya dunia, kupitia operesheni za mashambulizi na ulinzi zilizotekelezwa kwa mafanikio licha ya mashambulizi makali,”.

Aliongeza kuwa, kupitia usimamizi bunifu wa uwanja wa vita chini ya uongozi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatollah Sayyid Mojtaba Khamenei, na kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, vikosi hivyo vimefungua njia mpya za muqawama miongoni mwa watu wanaodhulumiwa duniani kote. Aidha, uwezo wao wa kulazimisha matakwa yao kwa adui umeelezwa kuwa ni ushahidi kwamba mfumo wa Kiislamu unaweza hatimaye kupata ushindi duniani kote.

Marekani na utawala wa Israel walianzisha vita vyao vya uchokozi dhidi ya Iran, kinyume cha sheria, mnamo Februari 28. Hata hivyo, siku arobaini tu baadaye, tarehe 8 Aprili, wavamizi hao walilazimika kukubali kusitisha mapigano, kutokana na msimamo thabiti wa Iran wa kupinga mashambulizi hayo pamoja na operesheni zake za kulipiza kisasi zilizokuwa na ufanisi mkubwa.