-
Ethiopia yazituhumu Eritrea, Sudan na Misri kwamba, zinawaunga mkono wanamgambo wa Tigray
Sep 30, 2026 11:46Ethiopia imezituhumu Eritrea, Sudan na Misri kuwa zinawaunga mkono wanamgambo wa Tigray, hatua ambayo Addis Ababa inaiona kuwa tishio kwa usalama na utulivu wa nchi.
-
Rais wa Afrika Kusini ataka hatua zichukuliwe kuwalinda wanawake baada ya kupatikana miili yao11 iliyotupwa
Sep 30, 2026 02:57Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amesema ametoa agizo la kufanyika operesheni ya kusafisha maeneo ya manispaa yenye hatari kubwa na kuchukuliwa hatua kali dhidi ya matumizi mabaya ya pombe ili kuwalinda wanawake, kufuatia mfululizo wa mauaji uliosababisha malalamiko na hasira nchi nzima.
-
Tume ya uchaguzi ya Kenya kusajili raia waishio katika nchi 26 kwa ajili ya uchaguzi wa 2027
Sep 29, 2026 11:54Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC) imepanua usajili wa raia wa nchi hiyo wanaoishi ughaibuni kutoka nchi 12 hadi 26, hatua inayolenga kuwapa Wakenya wengi zaidi nafasi ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa Agosti 2027.
-
Serikali ya Somalia: Mashambulizi ya kigaidi Mogadishu yamepeungua kwa 90%
Sep 29, 2026 03:03Waziri wa Ulinzi wa Somalia Ahmed Moallim Fiqi ametangaza kuwa, mashambulizi ya kigaidi katika mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu yamepungua kwa karibu asilimia 90 katika miaka ya hivi karibuni. Fiqi amesema, ripoti ya tathmini ya usalama iliyowasilishwa katika makao makuu ya Wizara ya Ulinzi katika wilaya ya Daynile jijini Mogadishu siku ya Jumamosi ilionyesha kuwa mashambulizi ya kigaidi yamepungua kwa takribani asilimia 87.
-
Vikosi vya Haftar vimenyonga watu 30 mashariki mwa Libya, wengine 50 hatarini kufikwa na hatima hiyohiyo
Sep 29, 2026 02:59Watu wasiopungua 30 wameuawa kwa kunyongwa mashariki mwa Libya tangu mwishoni mwa mwezi Agosti baada ya kuhukumiwa kifo katika kesi zilizoendeshwa kwa siri kupitia mahakama za kijeshi huku wengine wapatao 50 nao pia wakiwa wanakabiliwa na hatari ya kunyongwa.
-
UN yahimiza kuongezwa misaada na ufadhili kwa mataifa ya Pembe ya Afrika kukabiliana na El Nino
Sep 28, 2026 07:58Afisa mmoja mwandamizi wa Umoja wa Mataifa ametoa mwito wa kuunganishwa rasilimali za mataifa ya dunia ili kukabiliana na mgogoro unaozidi kuwa mbaya katika eneo la Pembe ya Afrika na tishio la El Nino.
-
Wanamgambo 12 wa al-Shabab waangamizwa katika operesheni maalumu nchini Somalia
Sep 28, 2026 02:47Shirika la Taifa la Ujasusi na Usalama la Somalia (NISA) limetangaza kuwa limefanikia kuangamiza wanamgambo 12 wa al-Shabab katika operesheni maalumu iliyofanyika kwenye eneo la kusini-kati la nchi hiyo.
-
Jeshi la Ethiopia laahidi kujizuia huku hofu ya vita vipya vya wenyewe kwa wenyewe ikiongezeka
Sep 27, 2026 12:55Jeshi la Shirikisho la Ethiopia limesema linashughulikia kwa utulivu na kujizuia hali ya mvutano unaoongezeka kaskazini mwa nchi hiyo, huku hofu ikizidi kwamba Ethiopia huenda ikatumbukia katika vita vingine vya wenyewe kwa wenyewe.
-
Watu wasiopungua 27 wauawa katika matukio mawili ya ufyatuaji risasi Johannesburg Afrika Kusini
Sep 27, 2026 12:06Polisi nchini Afrika Kusini imesema kuwa, kwa akali watu 27 wameuawa katika mashambulizi mawili tofauti ya ufyatulianaji risasi mjini Johannesburg.
-
Umoja wa Mataifa waonya kuhusu athari za mapigano mapya Tigray, Ethiopia
Sep 27, 2026 02:52Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, ameonya kuhusu athari za ongezeko la mapigano nchini Ethiopia.