Msemaji wa IRGC: Majibu ya Iran yamemtia kiwewe Donald Trump
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i137260-msemaji_wa_irgc_majibu_ya_iran_yamemtia_kiwewe_donald_trump
Msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amejibu upuuzi na uongo wa Rais Donald Trump wa Marekani akisema: "Rais muongo wa Marekani ametoa madai ya kumaliza nguvu ya vikosi vya jeshi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ili kujaribu kukwepa mashinikizo ya vita na kukomesha hali ya kukata tamaa wanajeshi wa Marekani katika eneo la Asia Magharibi."
(last modified 2026-03-10T04:14:15+00:00 )
Mar 10, 2026 04:14 UTC
  • Kamanda Ali Naeini
    Kamanda Ali Naeini

Msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amejibu upuuzi na uongo wa Rais Donald Trump wa Marekani akisema: "Rais muongo wa Marekani ametoa madai ya kumaliza nguvu ya vikosi vya jeshi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ili kujaribu kukwepa mashinikizo ya vita na kukomesha hali ya kukata tamaa wanajeshi wa Marekani katika eneo la Asia Magharibi."

Kamanda Ali Naeini ameongeza kuwa: "Baada ya kushindwa kwa aibu vitani, mhalifu Trump anatumia ujanja na udanganyifu ili kutengeneza mafanikio katika medani ya vita, kuhadaa maoni ya umma, na kuepuka mashinikizo ya kisaikolojia. Hatujaona chochote ila uongo kutoka kwa Trump."

Msemaji wa IRGC amesema: "Rais wa Marekani amedai kwamba meli za kibiashara na kijeshi zipo na zinavuka kirahisi katika eneo la Asia Magharibi kupitia Mlango-Bahari wa Hormuz, ilhali meli na ndege zote za kivita za Marekani zimekimbia eneo hilo na kwenda umbali wa zaidi ya kilomita 1,000 ili kujilinda kutokana na makombora na ndege zisizo na rubani zenye nguvu kubwa za Iran." Amesema, wanajeshi waoga wa Jeshi la Wanamaji la Trump wamekimbilia umbali wa zaidi ya kilomita 1,000 baada tu ya kurushwa makombora manne kwenye meli ya kivita ya USS Abraham Lincoln.

Kamanda Naeini ameongeza: "Trump anadai kuwa wanajeshi wake katika eneo la Asia Magharibi wako katika hali ya kawaida na bora, huku wanajeshi wa Marekani wakikimbia kambi zao wakiwa na mikoba yao ya mgongoni na kuhamishiwa katika miji mbalimbali ya kanda hii, na baadhi wamekimbilia mahotelini."

Amesema kwa upande wa Israel, wanajeshi wa utawala huo wamejificha miongoni mwa wananchi na vituo vya kiraia, wakitengeneza ngao za kibinadamu kwa ajili ya kubakia hai.

Amekumbusha kwamba: Trump alitaka kuwamimina wananchi wa Iran mitaani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu na kuisambaratisha Iran kijamii, lakini sasa amezabwa kibao kikali kutoka kwa watu wanaojielewa wa Iran, na hasira na hisia za kulipiza kisasi za Wairani dhidi ya Trump na mhalifu Netanyahu zinaendelea kupamba moto zaidi.

Jenerali Ali Naeini amesema: Trump alifanya jitihada za kuimaliza Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kuipigisha magoti kutokea ndani kwa muda mfupi kadiri iwezekanavyo na kwa gharama ya chini kabisa kupitia njia ya kuwaua viongozi wa Iran na makamanda wakuu wa kijeshi. Hata hivyo, uteuzi imara wa Kiongozi Mkuu wa Iran na usimamizi mzuri wa vita wa makamanda wa jeshi umemtia kiwewe na kumkatisha tamaa na kuwafanya washirika wake wakose matumaini kuhusu uwezekano wa kuanguka Jamhuri ya Kiislamu.