-
Baghaei: Vikwazo vya Marekani dhidi ya Wairani ni jinai dhidi ya ubinadamu
Nov 07, 2025 06:54Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, vikwazo vya Marekani dhidi ya Wairani ni jinai dhidi ya ubinadamu.
-
Araghchi: Tunaendelea kufungua milango ya masoko ya kimataifa kwa Iran
Nov 07, 2025 03:47Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, wizara yake inaendelea na jitihada zake za kidiplomasia za kufungua milango ya masoko ya kimataifa kwa ajili ya Iran na kuwasahilishia mambo wale wote wanaojishughulisha na masuala ya kiuchumi.
-
Qalibaf: Iran na Pakistan zinatoa kipaumbele kwa uhusiano wa kiuchumi na kibiashara
Nov 06, 2025 11:14Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amesema kuwa kupanua uhusiano wa kiuchumi na kuzidisha kiwango cha biashara kati ya Tehran na Islamabad ni vipaumbele vya juu vya nchi zote mbili.
-
Je, dunia inapaswa kuwa na wasiwasi juu ya uamuzi wa nyuklia aliotangaza Trump? Nini mtazamo wa Iran?
Nov 06, 2025 08:50Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa mjibizo kwa matamshi ya Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu kuanza tena nchi hiyo kuzifanyia majaribio silaha zake za nyuklia.
-
Rais wa Iran: Marekani na Ulaya lazima zionyeshe “uaminifu wa dhati”
Nov 06, 2025 07:53Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Masoud Pezeshkian, ameitaka Marekani na nchi za Ulaya kuonesha uaminifu wa dhati endapo zinataka kurejesha imani na Iran.
-
Araqchi: Iran iliilazimisha Marekani na Israel 'kusitisha mapigano bila masharti' badala ya 'kusalimu amri bila masharti'
Nov 06, 2025 04:04Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran amesifu kusimama kidete kwa nchi dhidi ya uvamizi wa hivi karibuni wa siku 12 wa Marekani na Israel, akisema kusimama kidete huko kulimlazimisha adui aliyetaka Iran ijisalimishe bila masharti, kuomba kusitishwa mapigano bila masharti.
-
Maonesho ya 16 ya Teknolojia ya Nano ya Iran yafanyika Tehran
Nov 05, 2025 12:36Maonesho ya 16 ya Teknolojia ya Nano ya Iran yamefanyika katika Uwanja wa Maonesho wa Kimataifa jijini Tehran, yakileta pamoja zaidi ya kampuni 150 za kiteknolojia.
-
Qalibaf: Vita vya siku 12 vimethibitisha kuwa 'uadui' wa Marekani dhidi ya Iran 'unaendelea'
Nov 04, 2025 12:48Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Baqer Qalibaf, ametangaza kwamba vita vya hivi karibuni vya siku 12 vimefichua uadui unaoendelea wa Marekani, akisisitiza kwamba ingawa mbinu zake zimebadilika, lakini lengo lake la msingi la kupinga Iran yenye nguvu na huru bado halijabadilika.
-
Tehran yasema 'vita halisi vya kikanda' na Israel vinaendelea, yapuuza mazungumzo na Marekani
Nov 04, 2025 11:37Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Iran amesema kwamba eneo la Magharibi mwa Asia kwa sasa limo katika na "vita halisi" na utawala wa Israel, akisisitiza kwamba hali ya eneo hilo iimekwenda mbali zaidi ya vitisho tu.
-
Tarehe 13 Aban; dhihiriisho la mshikamano wa kitaifa kwa ajili ya kukabiliana na sera za uingiliaji kati za Marekani nchini Iran
Nov 04, 2025 10:32Tarehe 13 Aban (4 Novemba) inafahamika katika kalenda ya Iran kama "Siku ya Taifa ya Kupambana na Uistikbari Duniani".