IRGC: Kama Netanyahu hajafa tutaendelea kumuwinda na kumuua
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i137374-irgc_kama_netanyahu_hajafa_tutaendelea_kumuwinda_na_kumuua
Idara ya Mawasiliano ya Umma ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (IRGC) imetangaza kuwa kama Waziri Mkuu mtendajinai wa Israel atakuwa hai jeshi hilo linamuwinda na kumuangamiza.
(last modified 2026-03-15T08:08:57+00:00 )
Mar 15, 2026 08:08 UTC
  • Waziri Mkuu mtendajinai wa Israel
    Waziri Mkuu mtendajinai wa Israel

Idara ya Mawasiliano ya Umma ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (IRGC) imetangaza kuwa kama Waziri Mkuu mtendajinai wa Israel atakuwa hai jeshi hilo linamuwinda na kumuangamiza.

Taarifa iliyotolewa na jeshi hilo imesema, kama Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel atakuwa bado yuko hai tutaendelea kumuwinda na kumpeleka jongomeo.

Sehemu moja ya taarifa ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu inasema: Shabaha za magaidi watendajinai wa Kimarekani na Kizayuni zimelengwa na kuharibiwa katika duru ya kwanza ya kulipiza kisasi cha damu ya wafanyakazi wa kitongoji cha viwanda cha Iran kwa kupiga maeneo kadhaa huko katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) na kambi tatu za Marekani katika eneo la Asia Magharibi kupitia operesheni mseto ya vikosi vya IRGC. Mashambulizi hayo yamefanyika katika wimbi la 52 la Operesheni Ahadi ya Kweli 4 kwa jina la msimbo la "Yaa Zainab (as)".

IRGC imeongeza kuwa: Sauti za ving’ora vya ambulansi na kukiri kwa taasisi za Kizayuni kwamba idadi ya Wazayuni waliouawa na kujeruhiwa katika mashambulizi ya Iran imeongezeka, vinadhihirisha ukubwa wa vipigo vya makombora ya IRGC katika kitongoji cha viwanda huko Tel Aviv.

Kitongoji cha viwanda na kituo cha majeshi ya Marekani katika kambi ya Anga ya al Harir huko Erbil na vilevile kambi za kijeshi za Ali al Salim na Arifjan pia zimepigwa kwa makombora na ndege zisizo na rubani.

Taarifa ya IRGC imesema: Kutokujulikana hatima ya Waziri Mkuu mtendajinai wa Israel na uwezekano kwamba ameuawa au ametoroka ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu yeye na watu wa familia yake, kunaonyesha mgogoro na mtikisiko ulioibuka baina ya wazayuni.

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu limesisitiza kuwa: Kama muuaji huyo wa watoto atakuwa bado yuko hai tutaendelea kumuwinda kwa nguvu zote na kumuua.