Kiongozi Muadhamu ateua makamanda wapya katika nyadhifa mbalimbali za jeshi la Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i140576-kiongozi_muadhamu_ateua_makamanda_wapya_katika_nyadhifa_mbalimbali_za_jeshi_la_iran
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amefanya uteuzi mpya katika baadhi ya nyadhifa za juu za kijeshi nchini, huku akimteua Brigedia Jenerali Ahmad Vahidi kuwa Kamanda mpya wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).
(last modified 2026-08-11T03:40:48+00:00 )
Aug 11, 2026 03:24 UTC
  • Kiongozi Muadhamu ateua makamanda wapya katika nyadhifa mbalimbali za jeshi la Iran
    Kiongozi Muadhamu ateua makamanda wapya katika nyadhifa mbalimbali za jeshi la Iran

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amefanya uteuzi mpya katika baadhi ya nyadhifa za juu za kijeshi nchini, huku akimteua Brigedia Jenerali Ahmad Vahidi kuwa Kamanda mpya wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).

Uteuzi huo ni sehemu ya mabadiliko katika uongozi wa juu wa kijeshi hapa nchini, ambapo makamanda wapya wamepewa majukumu katika taasisi mbalimbali za kijeshi.

Katika amri sita tofauti zilizotolewa jana Jumatatu, Kiongozi Muadhamu Ayatullaah Sayyid Mojba Khamenei amefanya uteuzi mpya katika nyadhifa za juu za kijeshi  ambapo kwa mujibu wa uteuzi huo, Meja Jenerali Ali Abdollahi ameteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Iran, huku Brigedia Jenerali Kioumars Heidari akiteuliwa kuwa naibu wake.

Aidha, Meja Jenerali Ahmad Vahidi, ambaye amepandishwa cheo na kuwa Meja Jenerali, ameteuliwa kuwa Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).

Vilevile, Meja Jenerali Mostafa Izadi ameteuliwa kuwa naibu wa Kamanda Mkuu wa IRGC.

Admeri Ali Ozamaei ameteuliwa kuwa Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).

Wakati huo huo, Hojjatoleslam Hossein Taeb ameteuliwa kuwa Mkuu wa Taasisi ya Kujitolea ya Basij.

Kiongozi Muadhamu, ameeleza vipaumbele vitatu muhimu kwa Mkuu mpya wa Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, akisisitiza haja ya kuimarisha uwezo wa ulinzi na usalama wa majeshi ya nchi pamoja na vikosi vya kujitolea vya Basij.

Ayatullah Mojtaba Khamenei amesisitiza umuhimu wa kuimarisha uwezo wa kina, wa kisasa na unaoendana na mahitaji ya sasa katika nyanja za ulinzi na usalama wa Majeshi ya Iran na vikosi vya kujitolea vya Basij.

Aidha, ametoa wito wa kuwekwa mazingira yatakayowezesha majibu ya haraka, ya kimapinduzi na yenye ufanisi dhidi ya vitisho vya aina zote na katika viwango mbalimbali vinavyoweza kuikabili Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.