-
Muungano wa Waandishi wa Habari: Israel imewaua wanafamilia 706 wa waandishi wa habari huko Gaza
Dec 29, 2025 07:00Jeshi la Israel limewaua watu 706 kutoka familia za waandishi wa habari katika Ukanda wa Gaza tangu kuanza kwa vita vya mauaji ya kimbari mnamo Oktoba 7, 2023. Taarifa hii ni kwa kujibu wa ufuatiliaji na nyaraka za Muungano wa Waandishi wa Habari wa Palestina.
-
Kiongozi wa Yemen: Tutachukua hatua za kijeshi dhidi ya uwepo wowote wa Israel huko Somaliland
Dec 29, 2025 06:57Kiongozi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema kwamba uwepo wowote wa Israel huko Somaliland utatambuliwa kama shabaha ya kijeshi, kwa sababu ni uchokozi dhidi ya Somalia na Yemen na tishio la moja kwa moja kwa usalama wa kikanda ambalo lazima likabiliwe kwa hatua madhubuti.
-
Kanali Msaudia: Imarati inafanya njama za kuigawa vipande vipande Saudi Arabia + Video
Dec 29, 2025 06:23Kanali mmoja mstaafu wa jeshi la Saudia ametoa kauli kali ambayo haijawahi kushuhudiwa dhidi ya Muungano wa Falme za Kiarabu (Imarati) akisema kuwa, nchi hiyo ni mkono wa utawala wa Kizayuni unaofanya kazi ya kuzidhoofisha na kuziangamiza nchi za Kiarabu na hasa Saudi Arabia.
-
Katibu Mkuu wa Hizbullah: Kuupokonya silaha Muqawama ni mradi wa kuangamiza nguvu za Lebanon
Dec 29, 2025 03:21Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu nchini Lebanon ya Hizbullah amesema: "leo, Lebanon iko katikati ya dhoruba na mvurugiko wa utulivu kutokana na sera za Marekani na adui wa Kizayuni."
-
Russia yasisitiza haja ya kuundwa taifa huru la Palestina
Dec 28, 2025 06:44Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, Sergey Lavrov amesema kwamba, Moscow ingali inaunga mkono suuala la kuanzishwa kwa taifa huru la Palestina.
-
Kwa nini utawala wa Kizayuni unaogopa uhuru wa vyombo vya habari?
Dec 28, 2025 02:46Bunge la utawala ghasibu wa Israel (Knesset) limelipa idhini baraza la mawaziri la utawala huo kufunga kanali za televisheni za kigeni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu kwa muda wa miaka miwili ijayo, hata katika wakati wa amani bila ya amri ya mahakama.
-
Hamas: Kutambuana kati ya "Israel" na "Somaliland" ni mfano hatari
Dec 27, 2025 12:11Harakati ya Kiislamu ya kupigania ukombozi wa Palestina (Hamas) imetangaza leo Jumamosi upinzani wake dhidi ya tangazo la utawala uliojitenga na Somalia katika eneo la "Somaliland" la kutambuana rasmi na Tel Aviv, ikisisitiza kuwa hatua hiyo "ni mfano hatari na jaribio lililoshindwa la kupata uhalali bandia dola vamizi linalohusika katika uhalifu wa kivita na mauaji ya kimbari."
-
Muungano wa waandishi wa habari wa Palestina: Israel 'inawanyamazisha' waandishi habari kwa mashambulizi ya kimfumo
Dec 27, 2025 09:47Chama cha Waandishi wa Habari cha Palestina kimeulaani utawala wa Israel kwa kufuata sera ya kimfumo ya kuwalenga waandishi wa habari, kikisema ukatili unaofanywa dhidi ya vyombo vya habari umeongezeka sana mwaka 2025 kama sehemu ya njama za kuzuia ripoti za Wapalestina.
-
Umoja wa Mataifa: Kujengwa vitongoji vipya Ukanda wa Gaza ni ukiukwaji wa wazi wa sheria za kimataifa
Dec 27, 2025 02:36Ripota maalum wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya kukuza nidhamu ya kidemokrasia na uadilifu kimataifa amesema kuwa, kauli za Waziri wa Vita wa Israel kuhusu kuanzishwa kwa vitongoji vipya katika Ukanda wa Gaza ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa.
-
Taasisi za Palestina: Maelfu ya wafungwa wanakabiliwa na mateso na njaa katika magereza ya Israel
Dec 27, 2025 02:24Asasi mbili za Kipalestina yametangaza kwamba, zaidi ya mateka na wafungwa 9,300 wa Palestina wanaoshikiliwa katika magereza na vituo vya kuzuiliwa vya Israel wanakabiliwa na "mateso yaliyopangwa."