Rais Pezeshkian akutana na Kiongozi Muadhamu anapoanza mwaka wake wa tatu madarakani
-
Rais Pezeshkian akutana na Kiongozi Muadhamu
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Masoud Pezeshkian, amekutana na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei, ikiwa ni mwanzo wa mwaka wake wa tatu tangu aingie madarakani.
Katika mazungumzo yao, wamejadili masuala mbalimbali muhimu yanayohusu uchumi na ulinzi wa nchi.
Mazungumzo hayo yaligusia mahitaji ya kimaisha ya wananchi, hali halisi na mwelekeo wa baadae wa vita vya chokochoko na uvamizi vinavyoendeshwa na Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Iran, maendeleo ya kijeshi, pamoja na mbinu za kulinda rasilimali na kudhibiti matumizi ya sarafu ya Rial, fedha za kigeni, nishati, na ushirikiano wa kiuchumi na washirika wa nje.
Mkutano huo unakuja wakati kukiwa na uwezekano wa kuongezeka kwa uhasama kati ya Iran na Marekani, baada ya upande wa pili (Marekani) kushindwa kufikia malengo yake iliyoyatangaza katika vita visivyo na msingi wowote dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel zilianzisha awamu yao ya pili ya vita dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu mnamo Februari 28. Vita hivyo vilianza kwa mauaji ya kigaidi dhidi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Shahidi Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, pamoja na makamanda na maafisa kadhaa wa ngazi za juu. Baada ya hapo Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei alichukua hatamu za uongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu
Mnamo Julai 6, 2024, Pezeshkian alichaguliwa kuwa rais baada ya kushinda duru ya pili ya uchaguzi wa rais wa mwaka 2024 uliotawaliwa Julai 5. Alipewa rasmi mamlaka ya urais na Ayatullah Sayyid Ali Khamenei mnamo Julai 28, 2024, na kuapishwa mbele ya bunge la Iran tarehe 30 Julai. Uchaguzi wake ulikuja miezi kadhaa baada ya Rais wa zamani Ebrahim Raeisi kufa shahidi katika ajali ya helikopta.