Jul 21, 2024 11:03
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameiasa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) idumishe maingiliano yenye kujenga na uongozi wa Rais mteule wa Jamhuri ya Kiislamu, Masoud Pezeshkian na kusema kuwa, mafanikio ya Rais mpya wa Iran ya Kiislamu ni mafanikio ya taifa hili zima.