Wanamichezo wa Iran wamkingia kifua Kiongozi Muadhamu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i136136-wanamichezo_wa_iran_wamkingia_kifua_kiongozi_muadhamu
Zaidi ya wanachama 5,000 wa jumuiya ya michezo ya Iran wametoa taarifa kulaani vitisho na bwabwaja za Rais wa Marekani Donald Trump, wakitangaza uungaji mkono wao mkubwa kwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei.
(last modified 2026-02-01T09:32:42+00:00 )
Feb 01, 2026 09:32 UTC
  • Wanamichezo wa Iran wamkingia kifua Kiongozi Muadhamu

Zaidi ya wanachama 5,000 wa jumuiya ya michezo ya Iran wametoa taarifa kulaani vitisho na bwabwaja za Rais wa Marekani Donald Trump, wakitangaza uungaji mkono wao mkubwa kwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei.

Taarifa hiyo, iliyosainiwa na maelfu ya wanariadha, wakufunzi, maveterani, maafisa wa michezo na wakurugenzi leo Jumapili, imelaani vikali matamshi ya vitisho ya Trump, ikiyaita ishara ya kukatishwa tamaa mbele ya umoja na uongozi wa kitaifa wa Iran. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wanariadha na wanamichezo wa Iran, wakiongozwa na mafundisho ya Kiislamu na urithi wa mashahidi, wanajitazama kama walinzi wa heshima ya taifa, izza na uhuru wa Jamhuri ya Kiislamu. Imesisitiza kwamba, michezo nchini Iran imejikita katika maadili ya ushujaa, Muqawama, uadilifu na maadili ndani na nje ya uwanja.

Wakilaani vitisho vyovyote au matusi dhidi ya uongozi na taifa la Iran, wanamichezo hao wamethibitisha uaminifu wao usioyumba kwa Kiongozi Muadhamu, wakimwelezea Ayatullah Khamenei kama nembo ya umoja na nguvu ya taifa. Kadhalika wameonya kwamba, hatua yoyote ya uadui dhidi ya mamlaka ya kujitawala au uongozi wa Iran itakabiliwa na jibu kali. Jamii ya wanamichezo wa Iran pia imeangazia umoja wa kitaifa kama silaha bora zaidi ya Jamhuri ya Kiislamu dhidi ya mashinikizo na njama za maadui, ikitaja ghasia za hivi karibuni hapa nchini kama ushahidi wa ustahimilivu wa pamoja.

Wakihitimisha taarifa hiyo, wametangaza utayarifu wao kamili wa kujitolea katika kuilinda Iran, maadili yake ya Kiislamu na thamani za Mapinduzi, wakisisitiza kwamba historia itahukumu maneno ya vitisho ya Rais wa Marekani, huku watu wa Iran wakiendelea kusimama imara katika kila uwanja.