Hizbullah: Vitisho vya US dhidi ya Kiongozi Muadhamu vitateketeza eneo lote
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i135828-hizbullah_vitisho_vya_us_dhidi_ya_kiongozi_muadhamu_vitateketeza_eneo_lote
Tawi la Kisiasa la Harakati ya Muqawama ya Hizbullah katika Bunge la Lebanon limeonya kwamba, vitisho vya maneno vya Marekani dhidi ya Iran na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei vinaweza kushadidisha mvutano katika eneo la Asia Magharibi.
(last modified 2026-01-24T03:31:56+00:00 )
Jan 24, 2026 03:31 UTC
  • Hizbullah: Vitisho vya US dhidi ya Kiongozi Muadhamu vitateketeza eneo lote

Tawi la Kisiasa la Harakati ya Muqawama ya Hizbullah katika Bunge la Lebanon limeonya kwamba, vitisho vya maneno vya Marekani dhidi ya Iran na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei vinaweza kushadidisha mvutano katika eneo la Asia Magharibi.

Taarifa ya ofisi hiyo ya kisiasa ya Hizbullah imeeleza wasiwasi wake kuhusu sera za kuchupa mipaka za Washington dhidi ya nchi za eneo hili, ikimkosoa Rais wa Marekani, Donald Trump kwa kutishia kuangamiza mataifa ya eneo na kubadilisha serikali zao.

"Uchokozi wa Marekani dhidi ya mataifa na watu katika eneo letu umefikia kiwango cha kiburi, na hata kutishia maisha ya Kiongozi Mkuu wa Kidini wa mamilioni ya Waislamu, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei," imesema.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, "Hili linatishia kuwasha moto katika eneo lote, na kuongeza tisho dhidi ya wananchi wa Iran ambao wamesimama kidete dhidi ya majaribio ya Marekani na Wazayuni ya kudhoofisha usalama na utulivu wao."

Kambi hiyo ya wabunge ya Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imesisitiza kuwa, inasimama upande wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, watu wake, na uongozi wake.

Aidha imempongeza Ayatullah Khamenei kwa "uongozi wake wa busara na ushujaa," ikisema, Kiongozi Muadhamu anayapa matumaini mataifa yaliyokandamizwa, katika juhudi zao za kukabiliana na dhulma duniani kote.

Kadhalika Ofisi ya Kisiasa wa Harakati ya Muqawama ya Hizbullah katika Bunge la Lebanon imepongeza maandamano ya kijasiri ya "watu milioni moja" ya Wairani mnamo Januari 12, ambayo yalizima njama za maadui za kuivuruga nchi hii.