-
Nyaraka za jeshi la Israel zafichua: Mfungwa wa Kipalestina aliyebakwa alikuwa raia, si mpiganaji
Nov 04, 2025 11:18Waraka wa siri wa jeshi la Israel umefichua kwamba mtu aliyeshambuliwa kikatili na kubakwa na kundi la wanajeshi wa Israel katika gereza maarufu la Sde Teiman mnamo Julai mwaka jana hajawahi kushtakiwa kwa uhalifu wowote na alikuwa raia, kinyume na madai kwamba alikuwa na mwanachama harakati za mapambano ya Hamas.
-
Israel inatumia wanasesere waliotegwa mabomu kuua watoto wachanga huko Gaza
Nov 04, 2025 10:20Wizara ya Afya ya Serikali ya Palestina katika Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel umetega mabomu kwenye wanasesere ili kuwaua watoto wa Palestina.
-
Duru za Israel: Hizbullah imeshajijenga upya, sasa tusubiri vita
Nov 04, 2025 07:00Mashirika ya usalama ya Israel yametangaza kwamba yanajiandaa kwa ajili ya kuingia kwenye vita vikubwa na Hizbullah ya Lebanon yakidai kuwa harakati hiyo imeshajijenga upya kijeshi na sasa lazima wasubiri majibu makali kutoka kwa harakati hiyo.
-
Majasusi watano wa Israel watiwa mbaroni Ghaza
Nov 04, 2025 07:00Kikosi cha kujihami kiitwacho "Rad'e" kinachoshirikiana na Muqawama kwa ajili ya kulinda usalama huko Ghaza, jana Jumatatu kilifanya operesheni ya kiusalama kusini mwa mji wa Khan Yunis na kuwatia mbaroni majasusi watano wa Israel.
-
Waziri al Sudani: Wananchi wataendelea kubeba silaha madamu Marekani bado ipo Iraq
Nov 04, 2025 06:58Waziri Mkuu wa Iraq, Mohammed al-Sudani alisema jana Jumatatu kwamba kuondoka kikamilifu Marekani na muungano wake unaodaiwa wa kupambana na Daesh huko Iraq ndiko kutakakopelekea kupokonywa silaha makundi ya kujihami ya wananchi. Kwa mujibu wa makubaliano, Marekani lazima iondoke Iraq mwezi Septemba mwaka ujao wa 2026.
-
UNICEF yaonya kuhusu mzozo wa kibinadamu kwa watoto Gaza licha ya kusitishwa mapigano
Nov 04, 2025 02:26Msemaji wa Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) ameashiria hali mbaya inayowakabili zaidi ya watoto milioni moja huko Gaza, ambao wanaendelea kuhitaji chakula na maji kwa dharura.
-
Israel yaandaa muswada wa 'kifashisti' wa kuruhusu utoaji wa hukumu ya adhabu ya kifo kwa Wapalestina
Nov 04, 2025 02:25Kamati moja ya wabunge wa utawala wa kizayuni wa Israel imeidhinisha muswada wa kuanzisha utoaji wa adhabu ya kifo kwa Wapalestina wanaoshikiliwa kwenye magereza ya utawala huo, na kufungua njia ya kusomwa hoja hiyo kwa mara ya kwanza bungeni licha ya kuandamwa na lawama nyingi.
-
Tetemeko la ardhi laikumba Afghanistan, makumi waripotiwa kufariki dunia
Nov 03, 2025 10:06Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.3 kwa vipimo vya richter limeikumba Afghanistan usiku wa kuamkia leo na kusababisha vifo vya makumi ya watu.
-
Umuhimu wa kusimama kidete Muqawama wa Lebanon katika kukabiliana na njama za Marekani na Israel
Nov 03, 2025 09:49Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu wa Lebanon Hizbullah Sheikh Naim Qassem, amesisitiza kuwa Hizbullah haitasalimu amri kwa vitisho vya Marekani kwa sababu nchi hiyo si mpatanishi asiyeegemea upande wowote na inaunga mkono utawala wa Kizayuni na uvamizi wa Israel.
-
Israel imeshakanyaga mara 194 makubaliano ya kusitisha vita Ghaza
Nov 03, 2025 06:34Ofisi ya Vyombo vya Habari ya Ghaza imetangaza kwamba jeshi vamizi la Israel limeshakanyaga mara 194 makubaliano ya kusitisha vita huko Ghaza yaliyofikiwa tarehe 10 Oktoba kwa ajili ya kumaliza mauaji ya kimbari ya miaka miwili yaliyokuwa yanafanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi wa Ghaza.