Pars Today
Washiriki wa kikao cha viongozi wa nchi za Kiarabu na Kiislamu kilichofanyika mjini Riyadh, Saudi Arabia wamesisitiza umuhimu wa kuzingatiwa suala la Palestina kama kadhia kuu na kuwaunga mkono kwa dhati wananchi wa taifa hilo ili wapate haki zao za kitaifa na zenye uhalali.
Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel limeendelea kufanya jinai za mauaji ya kinyama katika Ukanda wa Ghaza kwa kuwaua shahidi Wapalestina 14 asubuhi ya leo waliokuwa wamepata hifadhi katika linalodaiwa na utawala huo kuwa ni "eneo salama" huko al-Mawasi.
Harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina imetangaza katika taarifa kwamba, kauli ya Waziri wa Fedha wa utawala wa Kizayuni kuhusu kuukalia kwa mabavu Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan imewazaba kibao kingine wafanya mapatano.
Muqawama wa Kiislamu wa Iraq umetangaza kuwa umefanya shambulizi la ndege isiyo na rubani kwenye kituo cha kijeshi kusini mwa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu zilizopewa jina bandia la Israel.
Viongozi wa Kiislamu na wa Kiarabu ambao wameitisha mkutano wa dharura mjini Riyadh Saudi Arabia wameutaka utawala wa Kizayuni ukomeshe mara moja jinai zake za kinyama katika Ukanda wa Ghaza na Lebanon.
Msemaji wa Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, kukimbia wanajeshi wa utawala wa Kizayuni katika maeneo ya kusini mwa Lebanon ni ushahidi tosha wa udhaifu, kufeli na kushindwa wanajeshi hao na Muqawama wa Kiislamu.
Vikosi vya Ulinzi vya Yemen vimeendelea kuyatwanga kwa makombora maeneo tofauti ya utawala wa Kizayuni na kuzidi kuifedhehesha na kuidhalilisha mifumo ya ulinzi wa makombora ya Israel iliyogaiwa na madola ya kibeberu.
Mashirika ya kutetea haki za binaadamu yamelitaka Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA) kusitisha mchakato wa kuichagua Saudi Arabia kuwa mwenyeji wa michuano ya soka ya Kombe la Dunia mwaka 2034.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) amesemam kuwa kukaa kimya mkabala wa jinai zinazotekelezwa na utawala wa Israel dhidi ya wananchi wa Palestina na Lebanon ni sawa na kushiriki katika jinai hizo.
Harakatii ya Mapambano ya Hizbullah ya Lebanon kwa mara ya kwanza imekishambulia kwa makombora kituo cha ufuatiliaji wa kiufundi na kielektroniki cha utawala ghasibu wa Israel katika eneo la Golan linalokaliwa kwa mabavu.