-
UNICEF yaonya tena kuhusu utapiamlo miongoni mwa watoto wa Gaza
Sep 19, 2025 06:53Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) limetangaza kuwa zaidi ya watoto 26,000 katika Ukanda wa Gaza wanahitaji matibabu ya haraka kutokana na utapiamlo mkali.
-
Hamas yawataka walimwengu kushiriki siku za hasira za kimataifa dhidi ya Wazayuni
Sep 19, 2025 02:37Katika jitihada zake mpya za kuungwa mkono kimataifa wananchi wa Ghaza na wananchi wa Palestina kiujumla, harakati ya Hamas imetoa mwito kwa watu wote walio huru duniani kuzitangaza siku Ijumaa, Jumamosi na Jumapili kuwa siku za hasira za kimataifa dhidi ya Wazayuni wavamizi na wafuasi wao kupitia kukusanyika mbele ya balozi za nchi zote zinazoshiriki kwenye jinai za Ghaza.
-
Shambulio la Israel Doha laleta wasiwasi wa kugawika Misri vipande vipande
Sep 19, 2025 02:36Baada ya utawala wa Kizayuni wa Israel kufanya shambulio la kigaidi huko Doha, mji mkuu wa Qatar, Waziri Mkuu wa Misri amesema kwamba nchi yake nayo inalengwa katika njama za kuchora upya ramani ya eneo la Asia Magharibi na kuna hatari ikagawika vipande vipande.
-
Jinai kwa kinga; je, utawala wa Kizayuni unakanyaga vipi sheria za vita?
Sep 19, 2025 02:33Katika taarifa, Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas) imelaani vikali shambulio la jeshi la utawala ghasibu wa Israel dhidi ya raia karibu na hospitali ya Shafa, magharibi mwa Gaza na kulitaja kuwa jinai kubwa ya kivita.
-
Askari wanne wa utawala wa kizayuni waangamizwa, wanane wajeruhiwa kusini mwa Ghaza
Sep 18, 2025 10:42Vyanzo vya habari vimeripoti kuwa wanajeshi wanne wa utawala wa kizayuni wa Israel wameangamizwa na wengine wanane wamejeruhiwa katika mripuko wa bomu lililotegwa ardhini kusini mwa Ukanda wa Ghaza.
-
Balozi wa Marekani Israel: Israel ndiye mshirika wetu pekee wa kweli katika eneo la Mashariki ya Kati
Sep 18, 2025 10:12Balozi wa Marekani katika utawala wa kizayuni wa Israel, Mike Huckabee amesema, 'pamoja na Washington kuwa na washirika na marafiki kadhaa katika eneo la Mashariki ya Kati, "Israel ndiye mshirika wetu pekee wa kweli."
-
Israel yashadidisha mauaji dhidi ya wakazi wa Gaza; mashinikizo ya kimataifa yaongezeka dhidi yake
Sep 18, 2025 07:23Idadi ya vifo vya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza inaendelea kuongezeka huku mashambulizi ya kijeshi na mauaji ya kimbari ya Israel yakiingia mwaka wa pili sasa, na hivyo kuzidisha ukosoaji kimataifa.
-
Wabunge wa UK: Vikosi vya kijeshi vitakavyoongozwa na UN vipelekwe Ghaza kuzuia mauaji ya kimbari
Sep 18, 2025 03:46Wabunge watano wa Uingereza wamemwandikia barua waziri wao wa mambo ya nje Yvette Cooper wakiitaka serikali ya London "ifuatilie kwa dharura uingiliaji kati wa kijeshi utakaoongozwa na Umoja wa Mataifa" ili kukomesha mauaji ya kimbari ya yanayofanywa na Israel huko Ghaza.
-
Papa asema, Wapalestina wanahamishwa 'kwa mara nyingine tena' katika ardhi yao, ataka vita vya Ghaza vikomeshwe
Sep 18, 2025 03:45Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Leo XIV amesema Wapalestina wanaishi katika "mazingira yasiyokubalika" huku wakihamishwa kwa nguvu katika Mji wa Ghaza, wakati huu wa mashambulizi makubwa yanayoendelea kufanywa na jeshi la Israel.
-
Yemen yakosoa vikali Mkutano wa Doha kwa kushindwa kuchukua hatua kali dhidi ya Israel
Sep 17, 2025 12:50Serikali ya Yemen imekemea vikali viongozi wa Kiarabu na Kiislamu kwa kushindwa kuchukua hatua za kivitendo katika kuunga mkono Palestina na kukabiliana na jinai za utawala wa Kizayuni, ikisisitiza kuwa utawala huo wa kibeberu huelewa tu lugha ya nguvu.