-
Jeshi la Israel lavamia kusini mwa Syria baada ya 'makubaliano ya usalama' na HTS
Sep 17, 2025 12:01Jeshi la Israel limefanya uvamizi wa ardhini katika mkoa wa Quneitra, kusini magharibi mwa Syria, licha ya mazungumzo ya moja kwa moja yanayoendelea kati ya kundi la Hay’at Tahrir al-Sham (HTS) linalotawala Syria na utawala wa Israel kuhusu kile kinachodaiwa kuwa “makubaliano ya usalama.”
-
Wazayuni wakiri, mashambulizi ya makombora ya Iran yamezorotesha vibaya mno uchumi wa Israel
Sep 17, 2025 06:47Vyombo vya habari vya Kizayuni vimeifichua uhakika mpya kuhusu hasara waliyopata Wazayuni katika mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Iran yaliyopewa jina la "Operesheni ya Ahadi ya Tatu ya Kweli" na kusema kuwa, mashambulizi hayo yameisababishia Israel mdororo mkubwa mno wa kiuchumi.
-
Umoja wa nchi za Kiislamu, njia mwafaka ya kukabiliana na jinai za utawala wa Kizayuni
Sep 17, 2025 06:03Marais Abdel Fattah Al-Sisi wa Misri na Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wamesisitiza kuwa, kuimarishwa umoja na mafungamano baina ya nchi za Kiislamu ndiyo njia mwafaka zaidi ya kukabiliana na kukariri na kuendelea jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel katika eneo la Asia Magharibi.
-
Araqchi: Jumuiya ya ECO inapasa kuongoza katika kuasisi utaratibu mpya wa kiuchumi wa kikanda
Sep 17, 2025 02:20Abbas Araqchi Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amesema kuwa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi (ECO) inaweza na inapasa kuongoza na kutoa mchango athirifu katika kuunda utaratibu mpya wa kiuchumi katika eneo la Asia Magharibi.
-
Umoja wa Mataifa: Israel imetenda jinai za kivita Ukanda wa Ghaza
Sep 17, 2025 02:19Tume ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa imetangaza kwamba Israel imefanya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina katika Gaza.
-
Kumbukumbu ya miaka 43 ya mauaji ya Sabra na Shatila yaliyofanywa na Israel na kuitikisa dunia
Sep 16, 2025 12:06Mauaji ya Sabra na Shatila ni mfano mmoja tu wa jinai za kutisha zilizofanywa na utawala wa Israel huko Lebanon na kuitikisa dunia mwaka 1982, ambapo mauaji hayo leo yametimiza miaka 43.
-
Ghaza yaandamwa na mashambulio ya kiwendawazimu ya Wazayuni, wanakaribia kuikalia kikamilifu
Sep 16, 2025 07:03Jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel limeanzisha mashambulizi makali ya anga dhidi ya Mji wa Ghaza kwa saa kadhaa, ambapo mbali na kuwaua shahidi Wapalestina kadhaa linateketeza pia majengo na miundomsingi iliyosalia katika eneo hilo.
-
Kwa mara ya kwanza Netanyahu akiri kwamba Israel imenasa kwenye kinamasi cha 'kutengwa' kimataifa
Sep 16, 2025 06:47Waziri Mkuu wa utawala wa kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu amekiri kwa mara ya kwanza hadharani kwamba utawala huo ghasibu unatumbukia kwenye lindi la "kutengwa," wakati mashinikizo ya kimataifa yakiwa yanaongezeka dhidi ya vita vinavyoendelezwa na jeshi la kizayuni katika Ukanda wa Ghaza na dhidi ya sera za serikali ya Netanyahu ya mrengo wa kulia yenye misimamo mikali ya chuki na ubaguzi.
-
Namna Ghaza inavyowabebesha jinamizi la kiafya wanajeshi wa Israel
Sep 16, 2025 02:17Makumi ya wanajeshi wa utawala wa wa Kizayuni wa Israel waliovamia Ghaza wameambukizwa magonjwa ya ngozi ya kuambukiza.
-
UNRWA: Hakuna sehemu salama katika Ukanda wa Gaza
Sep 15, 2025 10:48Philippe Lazzarini, Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) amesema kuwa, hivi sasa hakuna sehemu salama huko Gaza na kwamba mashambulizi ya anga yanaendelea kushika kasi.