-
Mbunge wa Hizbullah: Israel haina uwezo wa kuufuta Muqawama, utaendelea kuwa thabiti
Sep 21, 2026 10:32Hassan Fadhlullah, mbunge wa Hizbullah katika Bunge la Lebanon na mwanachama wa mrengo wa Uaminifu kwa Muqawama katika bunge hilo, ametoa wito kwa wananchi kusimama imara na kuwa na subira na kusisitiza kwamba, kama alivyousia na kutilia mkazo Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah Muqawama utabaki kuwa thabiti na kwamba suala la kuufuta na kuuangamiza ni dhana na mawazo hewa tu.
-
Yemen kuendeleza mlingano wa "kuishambulia Riyadh mkabala wa Sana'a"; yatoa onyo pia kwa US
Sep 21, 2026 10:27Mkuu wa idara ya habari ya ofisi ya rais wa Yemen amesema, serikali ya Sana'a imedhamiria kuendeleza mlingano wa "Riyadh mkabala wa Sana'a" wa kuushambulia kijeshi mji mkuu wa Saudi Arabia mkabala wa kushambuliwa mji mkuu wa nchi hiyo Sana'a na kutoa onyo pia kwa serikali ya Marekani.
-
Netanyahu aungana na walowezi zaidi ya laki moja kuuvunjia heshima Msikiti wa Al-Aqsa
Sep 20, 2026 13:59Sambamba na Wazayuni zaidi ya 100,000 kuuvamia Msikiti Mtukufu wa Al-Aqsa, waziri mkuu wa utawala wa kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu naye pia ameungana na wazayuni hao katika kulivunjia heshima eneo hilo takatifu kwa kufika hadi kando ya ukuta wake wa Buraq na kwenye njia zake za chini kwa chini.
-
Na’im Qassem: Kukabiliana na utawala wa Israel kunawezekana tu kupitia muqawama
Sep 20, 2026 13:07Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, kukabiliana na ubeberu na utawala wa Israel kunawezekana tu kupitia muqawama na mapambano.
-
Mwanzo wa mwaka mpya wa masomo Gaza katika mahema; hali ni ngumu sana
Sep 20, 2026 04:27Takribani wanafunzi laki saba wanaoishi katika Ukanda wa Gaza huko Palestina wameanza mwaka mpya wa masomo katika mazingira magumu sana.
-
CPJ yalaani utekaji wa mwandishi wa Press TV na utawala wa Kizayuni, yadai aachiwe huru mara moja
Sep 19, 2026 11:47Kamati ya Kimataifa ya Kulinda Wanahabari (CPJ) imelaani vikali kitendo cha utawala wa Kizayuni wa Israel kumteka mwandishi wa habari wa Press TV, Bi. Naqaa Hamed, na imedai aachiwe huru mara moja.
-
Ripoti: Syria yakataa ombi la Saudia la kutuma mamluki dhidi ya vikosi vya Yemen
Sep 19, 2026 11:44Inaripotiwa kuwa kundi la Hay’at Tahrir al-Sham (HTS) linalotawala baadhi ya maeneo nchini Syria, limekataa ombi rasmi kutoka kwa utawala wa Saudia la kupanga na kuwapeleka mamluki na wanamgambo wa Kisyria nchini Yemen ili kupambana na Jeshi la Yemen, ambalo limekuwa likitoa vipigo vikali vya kijeshi dhidi ya mamluki wanaoungwa mkono na Saudia.
-
Saudia yakimbilia Oman kuomba kusimamishwa vita Yemen
Sep 18, 2026 10:38Baada ya kuanzisha vita vya miaka mingi kwa lengo la kuiteka Yemen, sasa hali ni ngumu sana kwa Saudi Arabia kiasi kwamba imefikia hatua ya kuomba msaada wa Oman iingilie kati ili kusimamisha mashambulizi ya Ansarullah na Jeshi la Yemen.
-
Al-Houthi: Madai ya Saudia kuwa Yemen imelenga Makkah ni “uongo wa kuchukiza,” na kashfa ya wazi
Sep 18, 2026 03:46Kiongozi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen, Sayyid Abdul-Malik al-Houthi, amelaani vikali madai ya Saudi Arabia kuwa vikosi vya Yemen vimelenga mji mtakatifu wa Makkah, akifutilia mbali madai hayo kama “uongo mkubwa, mbaya, na wa kuchukiza” unaolenga kuhalalisha vita vya Saudia dhidi ya Yemen.
-
Wanamgambo wa HTS wauawa Syria huku maandamano ya kupinga hali ngumu ya maisha yakisambaa
Sep 17, 2026 11:41Takriban wanamgambo watatu wanaofungamana na utawala unaotawala wa kundi la Hay’at Tahrir al-Sham (HTS) nchini Syria wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa, kufuatia mapigano makali yaliyozuka kati ya vikosi hivyo na wapiganaji wa kundi la wenyeji katika mkoa wa kusini-magharibi wa Dara’a.