Zaidi ya wanamichezo 1,000 wa Kipalestina wameuawa shahidi na Israel
-
Zaidi ya wanamichezo 1,000 wa Kipalestina wameuawa shahidi na Israel
Shirikisho la Soka la Palestina limetangaza kuwa wanamichezo 1,013 wa Kipalestina wameuawa shahidi tangu kuanza vita dhidi ya Ukanda wa Gaza mwezi Oktoba 2023, kutokana na mashambulizi ya utawala wa Kizayuni.
Katika taarifa yake, Shirikisho hilo limesema kuwa wanamichezo hao wamepoteza maisha wakati wa uhalifu wa kivita unaofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina.
Shirikisho hilo lilieleza kuwa mashambulizi hayo yameathiri kwa kiwango kikubwa sekta ya michezo huko Palestina, huku mamia ya wanamichezo, makocha na maafisa wa michezo wakiuawa au kujeruhiwa, pamoja na miundombinu ya michezo kuharibiwa. Israel ilianzisha vita vya mauaji ya kimbari huko Gaza mnamo Oktoba 7, 2023, baada ya kundi la muqawama la Hamas la Palestina kufanya operesheni ya kihistoria dhidi ya utawala huo ikiwa ni kulipiza kisasi jinai za miongo kadhaa za Wazayuni dhidi ya Wapalestina.
Takwimu zinaonyesha kuwa, idadi ya Wapalestina waliouawa shahidi tangu kuanza hujuma kinyama ya jeshi la utawala wa Kizayuni huko Gaza imepindukia 73,000.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, takribani asilimia 80 ya uwezo wa huduma za uokoaji na misaada ya dharura umeangamizwa kutokana na mashambulizi na uharibifu unaoendelea kufanywa na utawala ghasibu wa Israel katika Ukanda wa Gaza.
Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Dharura za Tiba katika Ukanda wa Gaza amesema kuwa tangu kuanza vita vya mauaji ya kimbari katika eneo hilo, utawala wa Kizayuni umefuata sera ya kimfumo ya kulenga wafanyakazi wa huduma za dharura, magari ya uokoaji, magari ya zimamoto, hospitali na vituo vya matibabu.
Kulengwa wahudumu wa afya na vifaa vya uokoaji kumesababisha kupungua kwa uwezo wa mifumo ya dharura kutoa huduma katika kipindi ambacho mahitaji ya matibabu yameongezeka kutokana na idadi kubwa ya majeruhi na uharibifu wa miundombinu.
Iran: Mashambulizi yataendelea hadi adui atakapojisalimisha kikamilifu