Kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam Ali bin Mussa al Ridha (AS)
https://parstoday.ir/sw/news/religion-i140638-kumbukumbu_ya_kuuawa_shahidi_imam_ali_bin_mussa_al_ridha_(as)
Siku kama ya leo miaka 1244 iliyopita, aliuawa shahidi Imam Ali bin Musa al Ridha AS, mmoja kati ya wajukuu wa Mtume Mtukufu SAW.
(last modified 2026-08-13T09:28:12+00:00 )
Aug 13, 2026 09:20 UTC
  • Kumbukumbu ya kuuliwa shahidi Imam Reza (AS)
    Kumbukumbu ya kuuliwa shahidi Imam Reza (AS)

Siku kama ya leo miaka 1244 iliyopita, aliuawa shahidi Imam Ali bin Musa al Ridha AS, mmoja kati ya wajukuu wa Mtume Mtukufu SAW.

Mtukufu huyo alizaliwa mwaka 148 Hijria katika mji wa Madina na alichukua jukumu la kuongoza Umma wa Kiislamu baada ya kuuawa shahidi baba yake, yaani Imam Mussa al Kadhim AS. Mnamo mwaka 200 Hijria, Maamun, Khalifa wa Bani Abbasi, alimtaka Imam Ridha AS aelekee kwenye makao ya Khalifa huyo yaliyokuwa katika mji wa Marwi, kusini mashariki mwa Turkemenistan ambayo ilikuwa sehemu ya Khorasan Kuu.

Ijapokuwa kidhahiri Maamun alimfanya Imam Ridha kuwa mrithi wake, lakini kwa njia hiyo alikusudia kuimarisha zaidi nguvu za utawala wake. Utukufu na daraja ya juu ya kielimu na kiroho ya Imam Ridha na ushawishi wake uliokuwa ukiongezeka siku baada ya siku ndani ya fikra na nyoyo za watu vilimtia woga na hofu Maamun na hivyo akaamua kufanya njama za kumpa sumu na kumuua shahidi mjukuu huyo wa Mtume katika siku kama leo.

Imam Ali bin Musa Ridha As ana lakabu nyingi, lakini iliyokuwa mashuhuri ni ile ya ar Ridha yaani shakhsia huyo aliridhia matakwa ya Mwneyezi Mungu SW; marafiki zake walimridhia na maadui zake hawakueleza sababu za kutomridhia yeye.

Haram ya Imam Ridha AS iko katika mji wa Mash'had kaskazini mashariki mwa Iran.