Ulyanov: Marekani imekuwa ikisubiri kuanguka uchumi wa Iran tangu 1980
https://parstoday.ir/sw/news/world-i141792-ulyanov_marekani_imekuwa_ikisubiri_kuanguka_uchumi_wa_iran_tangu_1980
Mwakilishi wa Kudumu wa Russia katika mashirika ya kimataifa ya mjini Vienna Austria, amejibu madai ya hivi karibuni ya waziri wa fedha wa Marekani na kusisitiiza kuwa "njia mbadala hazifanyi kazi" hivyo anaishauri Washington kutafuta njia za amani za kutatua masuala na Iran.
(last modified 2026-09-28T08:53:57+00:00 )
Sep 28, 2026 08:52 UTC
  • Ulyanov: Marekani imekuwa ikisubiri kuanguka uchumi wa Iran tangu 1980

Mwakilishi wa Kudumu wa Russia katika mashirika ya kimataifa ya mjini Vienna Austria, amejibu madai ya hivi karibuni ya waziri wa fedha wa Marekani na kusisitiiza kuwa "njia mbadala hazifanyi kazi" hivyo anaishauri Washington kutafuta njia za amani za kutatua masuala na Iran.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Fars, mwakilishi huyo wa Russia amesema hayo kupitia mtandao wa kijamii wa X kufuatia kauli za hivi karibuni za waziri wa fedha wa Marekani aliyedai kuwa uchumi wa Iran utaaanguka ndani ya wiki mbili. Ulyanov amesema kwamba, Marekani imekuwa ikitarajia kuanguka uchumi wa Iran tangu mwaka 1980 (baada ya ushindii wa Mapinduzi ya Kiislamu) lakini ndoto hiyo imeshindwa kuaguka hadi leo hii.

Mwanadiplomasia huyo mwandamizi wa Russia amesema ingekuwa bora kwa Marekani yenyewe, kwa eneo la Ghuba ya Uajemi na kwa dunia nzima kama Washington ingeamua hatimaye kuipa nafasi amani na utulivu.

"Njia mbadala hazifanyi kazi," amesema.

Jana waziri wa fedha wa Marekani, Scott Bessent alikariri madai ya uongo ya bosi wake yaani Trump kuhusu Lango-Bahari la Hormuz na kutoa kauli kuhusu mauzo ya mafuta ya Iran, akisema kuwa ni mapipa milioni 15 pekee ya mafuta ya Iran ndiyoi yaliyobakia katika usafirishaji baharini. Alidai kuwa shehena za mwisho huenda zikapelekwa China ndani ya wiki mbili zijazo, na baada ya hapo Iran haitakuwa na kitu chochote kilichosalia cha kuuza.

Upayukaji huo usio na mwisho wa viongozi wa Marekani unatolewa kwa hamaki zilizojaa vifuani mwao baada ya kushindwa kufikia malengo yao haramu katika vita dhidi ya Iran.

Baada ya kuona imeshindwa katika vita vya silaha za moto, Washington ilitangaza vita vya kiuchumi na kuongeza mashinikizo dhidi ya Tehran. Lakini Jamhuri ya Kiislamu imekuwa kwenye vikwazo hivyo kwa makumi ya miaka, na wataalamu wanaamini kuwa vikwazo hivi navyo vitashindwa tu kama yalivyoshindwa "mashinikizo ya juu zaidi" ya Washington dhidi ya Tehran.