-
CNN: Vita vya Iran vaisababishia Marekani hasara ya dola bilioni 3.3
Oct 10, 2026 03:56Televisheni ya CNN ya Marekani ambayo ni moja ya televisheni kubwa na za daraja la kwanza nchini humo imetangaza kuwa, vita vilivyoanzishwa na Washington dhidi ya Iran tarehe 28 Februari 2026 vimeisababishia Marekani hasara ya takriban dola bilioni 3.3.
-
Volker Türk: Madhara ya biashara ya utumwa wa Waafrika na ukoloni yanaendelea kuathiri maisha yao
Oct 09, 2026 03:10Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu, Volker Türk, amesema madhara ya biashara ya utumwa wa Waafrika na ukoloni yanaendelea kuathiri maisha ya Waafrika na watu wenye asili ya Afrika, yakichangia ukosefu wa usawa katika fursa, usalama na mamlaka.
-
Bei ya nishati ya mafuta yaendelea kupanda kutokana na mvutano katika Ghuba ya Uajemi
Oct 09, 2026 02:41Bei ya mafuta duniani iliendelea kupanda jana Alkkhamisi, kufuatia kuendelea wasiwasi kuhusu upatikanaji wa mafuta yanayozalishwa na nchi za Asia Magharibi, pamoja na kuongezeka mashambulizi dhidi ya meli katika Ghuba ya Uajemi na Mlango Bahari wa Hormuz.
-
CBS: Mashambulio ya 'kutisha' ya Iran yaliwafanya askari wa US 'waitelekeze' kambi ya Buehring, Kuwait
Oct 08, 2026 10:57Mashambulizi ya "kutisha" ya kulipiza kisasi ya Iran yaliyofanywa katika siku za awali za vita vya kichokozi vya Marekani na utawala wa kizayuni wa Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu, yalivilazimisha vikosi vya Marekani "kuitelekeza" Kambi ya Buehring (CBKU), ambayo ni kituo kikuu cha kijeshi cha Marekani nchini Kuwait.
-
Sanamu la Trump akiwa utupu lafanywa maonyesho kwenye jengo la Bunge la Ulaya
Oct 08, 2026 10:55Sanamu kubwa la dhahabu la Rais wa Marekani Donald Trump akiwa utupu limewekwa kwa ajili ya maonyesho ndani ya jengo la Bunge la Ulaya mjini Strasbourg, Ufaransa.
-
Gazeti la Pakistan: Serikali iepuke kujiingiza kwenye vita vya Yemen na kutuma askari wa nchi kavu
Oct 08, 2026 03:20Gazeti mashuhuri la Dawn la nchini Pakistan limezungumzia makubaliano ya hivi karibuni kati ya nchi hiyo, Saudi Arabia na Uturuki ya kupeleka wanajeshi haraka nchini Saudia, na kuitaka serikali ya Islamabad iepuke kujiingiza katika vita vya Yemen.
-
Askari wa US waliojeruhiwa katika shambulio la Iran wasema jeshi limewatelekeza
Oct 08, 2026 03:15Wanajeshi kadhaa wa Marekani waliojeruhiwa katika moja ya mashambulizi makali ya ndege zisizo na rubani yaliyofanywa na Iran nchini Kuwait wamesema mfumo wa matibabu wa jeshi umewatelekeza na kuwaacha bila ya kuwapatia matibabu ya kutosha.
-
Je, hatua za mabavu na kiusalama zinaweza kutatua mgogoro wa elimu nchini Ufaransa?
Oct 07, 2026 05:34Maandamano ya wanafunzi nchini Ufaransa yamevuka mipaka ya mzozo wa kawaida kuhusu elimu, na kuwa mtihani mkubwa kwa nchi hiyo ya Magharibi, ambapo umeanika hadharani madai yake ya uongo kuhusu suala la haki za binadamu, uhuru wa kuandamana na haki ya kukusanyika.
-
Mchambuzi maarufu amsuta Trump asema bei halisi ya mafuta ni dola 140 kwa pipa
Oct 07, 2026 02:59Licha ya Trump na mawaziri wake kujigamba kwamba mtiririko mkubwa wa mafuta kupitia Lango-Bahari la Hormuz na mabomba mbadala yamerekebisha mauzo ya mafuta ya Ghuba ya Uajemi, lakini uhalisia wa mambo ni kinyume na madai hayo kwani kwa mujibu wa taarifa za hivi karibuni, bei ya hivi karibuni zaidi ya mafuta ni dola 140 kwa pipa.
-
Mgogoro wa mafuta Marekani wazidi kuwa mbaya; Trump ageukia dizeli ya rangi nyekundu
Oct 06, 2026 11:38Rais wa Marekani, Donald Trump ametia saini amri ya kiutendaji inayopanua matumizi ya dizeli ya rangi nyekundu, ambayo kwa kawaida husamehewa kodi na hutumika katika shughuli zisizo za barabarani, kama vile kilimo na ujenzi.