Politico: Marekani inachukiwa sana kuliko Wamarekani wanavyodhani
Matokeo ya uchunguzi wa maoni yanaonyesha kuwa sura ya Marekani ni mbaya sana miongoni mwa raia wa nchi waitifaki wa nchi hiyo duniani kwa kiasi ambacho hakiingii hata katika fikra na akili za Wamarekani.
Matokeo ya uchunguzi wa maoni yaliyochapishwa kwenye tovuti ya habari ya Kimarekani, Politico, yanaonyesha kuwa, sura ya nchi hiyo duniani ni mbaya zaidi kuliko inavyodhaniwa na Wamarekani.
Uchunguzi huo wa maoni umeshirikisha watu katika nchi za Marekani, Canada, Ufaransa, Ujerumani na Uingereza katika kipindi cha baina ya tarehe 6 na 9 Februari na kujumuisha watu wazima 10,289.
Kwa mujibu wa uchunguzi huo wa maoni, idadi kubwa ya raia wa nchi waitifaki wa Marekani ikiwa ni pamoja na zaidi ya asilimia 43 ya Wacanada, wanaamini kwamba Marekani ni tishio kwa usalama wa dunia.
Vilevile raia wa nchi waitifaki na Marekani wanaamini kwa, haiwezekani kuitegmea Marekani katika vipindi vya migogoro.
Asilia 57 ya Wacanada, 51% ya Wajerumani, 47% ya Wafaransa na asilimia 42 ya Waingereza pia wana mtazamo kama huo kuhusu Marekani.