Dunia ya Siku Zijazo
Hebu, jaribu kufumba macho yako na faradhisha kuwa unaishi katika mwaka wa 2050. Kwa mtazamo wako dunia itakuwaje wakati huo? Mgawanyo wa nguvu umebadilika vipi?
Ulimwengu wa kambi moja yenye nguvu ambao uliundwa baada ya Vita Baridi ukiongozwa na Marekani, sasa unaonyesha dalili za mmomonyoko; kuanzia migawanyiko ya ndani nchini Marekani hadi kushindwa kwake kudhibiti changamoto za dunia.
Marekani imeshindwa kabisa kutatua changamoto mbalimbali kama vile kuidhibiti China, kupanua NATO kuelekea Mashariki, kuunda Mashariki ya Kati mpya inayoongozwa na Israel, na masuala mengine mengi.
Katika mfumo huu mpya, nguvu inabadilika na kuhama kutoka Magharibi kuelekea Mashariki. Kutoka kambi moja hadi kambi kadhaa za nguvu. Mabadiliko haya hayawahusu wachezaji tu, bali pia mantiki ya mchezo wenyewe.
Ikiwa mfumo wa zamani ulisimama kwenye msingi wa ubeberu na udhibiti wa kimabavu, leo "muqawama" unatoa changamoto kubwa kwa mfumo huo. Kuanzia Asia Magharibi hadi Amerika Kusini na hata Ulaya na Amerika Kaskazini, mataifa hayakubali tena kirahisi kutawaliwa na mfumo kandamizi na wa kutwishwa.
Kuhusu suala hili, nafasi ya Iran ni tofauti na ya wachezaji wengine. Iran daima imekuwa nchi yenye historia tajiri, nafasi ya kipekee ya kijeopilitiki na rasilimali watu ya kipekee.
Mbali na hayo, Mapinduzi ya Kiislamu na kuanzishwa kwa Jamhuri ya Kiislamu kuliipa hadhi maalumu zaidi. Kuondolewa nchini kwa mfumo wa udikteta na kukomeshwa ubeberu wa Marekani juu ya Iran ni miongoni mwa matokeo ya awali ya mapinduzi hayo.
Lakini Jamhuri ya Kiislamu haikuishia hapo, na tangu mwanzoni kabisa, katika kauli mbiu na matendo yake, ilitanguliza mbele uungaji mkono na sera ya kuyatetea mataifa yanayodhulumiwa duniani. Kwa kuunga mkono mataifa na makundi ya muqawama na mapambano ya ukombozi na kuanzisha mshikamano kati yao, Iran ya Kiislamu imeweza kusimamisha au kupunguza kasi ya miradi ya Marekani katika eneo la Asia Magharibi na dunia nzima kwa ujumla.
Huu ni mzozo wa kiustaarabu, ambapo katika njia hii Iran imekabiliwa na matatizo na njama nyingi kama vile vikwazo vya kiuchumi, mapinduzi laini, kugawanywa nchi, na vita vitatu vya kulazimishwa.
Pamoja na hayo, lakini Iran, imebadilika kuwa kigezo bora cha kimataifa, kutokana na mapambano yake endelevu.
Wachambuzi wa mambo wanaamini kwamba, iwapo mapambano na muqawama wa Iran na washirika wake utaendelea, ulimwengu unaokuja utakuwa ulimwengu usio na Marekani wala ubabe na ubeberu.