Rais Pezeshkian: Hatuogopi vita, lakini vita havina maslahi na mtu yeyote
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i139326-rais_pezeshkian_hatuogopi_vita_lakini_vita_havina_maslahi_na_mtu_yeyote
Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa: "Hatuogopi vita, lakini vita havina maslahi na mtu yeyote.
(last modified 2026-06-22T04:45:22+00:00 )
Jun 22, 2026 04:43 UTC
  • Rais Pezeshkian: Hatuogopi vita, lakini vita havina maslahi na mtu yeyote

Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa: "Hatuogopi vita, lakini vita havina maslahi na mtu yeyote.

Rais Pezeshkian alisema hayo jana katika Kongamano la 33 la Sera ya Fedha na Benki mjini Tehran, na kubainisha kwamba, "Vita havina maslahi na mtu yeyote, na kuendelea kwake hakutanufaisha kundi lolote.Utafiti wa kimataifa pia unakubali kwamba vita huzuia ukuaji wa uchumi na maendeleo na kueneza umaskini. Hii haimaanishi kwamba tunaogopa vita. Wanajeshi wa Iran na wananchi wa Iran wameonyesha kuwa wamesimama imara na wataendelea kupigana kwa nguvu iwapo vita hivyo vitaendelea.

Rais Pezeshkian ameeleza kuwa, vipengee vya hati ya maelewano kati ya Iran na Marekani kimsingi ni kwa maslahi ya taifa la Iran na kuongeza kuwa: "Marekani inataka kuhakikisha kwamba hatuna bomu la atomiki. Suala hili pia limetiliwa mkazo na kiongozi aliyeuawa shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, na tumelisisitiza mara nyingi.

Wakati huo huo, Rais wa Iran amesema kuwa, Waziri Mkuu wa utawala wa kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu ndiye mpinzani mkuu wa mazungumzo yanayoendelea kati ya Tehran na Washington yenye lengo la kuhitimisha vita katika eneo hili kwa sababu hataki eneo hili liwe na amani na utulivu.

Rais Pezeshkian anaziona jinai zinazofanywa hivi sasa na utawala wa Kizayuni huko Lebanon na Ghaza kuwa sehemu ya njama ya kuendeleza machafuko katika eneo hili na pia kuizuia Iran kupata mali zake, kutatua matatizo yake na kupanua uwezo wake.